Steven William Muheza
WAKAZI 16 wanaoishi katika kijiji cha Kicheba Kata ya Kicheba wilayani Muheza walifika katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Muheza wakingojea kulipwa fidia zao za mazao kutokana na mwekezaji kuchukuwa mashamba yao kwa ajili ya kujenga Chuo cha Ufundi Stadi (VETA).
Juzi asubuhi wakazi hao walikuwepo katika viwanja vya Halmashauri wakiwa wamekaa chini ya mti wakimsubiri mwekezaji huyo kutoka jijini Dar es salaam afike ili walipwe fidia zao.
Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi Mwenyekiti wa Kijiji cha Kicheba Hiza Ramadhani alisema kuwa mashamba yao yalichukuliwa na mwekezaji ambaye alimtaja kwa jina la John Chagama ambaye anataka kujenga Chuo cha Ufundi Stadi (VETA).
Mwenyekiti huyo alisema kuwa watu ambao watalipwa fidia wapo 16 ambapo watalipwa mazao yao ambayo yapo mashambani.Alisema kila mtu atalipwa kulingana na mimea yake ambayo yapo shambani kwake ili aridhike mwenyewe.
Mwenyekiti huyo alisema mwekezaji huyo alishafanya malipo ya mara ya kwanza kwa watu wengine ambapo aliwalipa zaidi ya Milioni 10.7 kama fidia ya mimea yao.
Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho walifurahia mpango mzuri wa mwekezaji huyo kujenga chuo cha VETA katika eneo hilo la Kicheba kwani watoto watajifunza ufundi na kujiajiri wenyewe.
Chanzo: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment