Home » » Bumbuli wamshukuru January Makamba kwa kutatua kero,waahidi kumchagua tena

Bumbuli wamshukuru January Makamba kwa kutatua kero,waahidi kumchagua tena

Wakizungumza wakati wa ziara ya Mbunge huyo ya kusikiliza kero na kutoa majawabu aliyoifanya katika kila kijiji cha jimbo hilo, wananchi wamesema jitihada anazozifanya Mbunge wao kutatua changamoto katika sekta zote, wanasisitiza kuwa lazima wamchague tena.


" Sisi wananchi wa Bumbuli hatuna deni na wewe kwa sababu umetufanyia mengi, tena mengine kwa pesa zako za mfukoni. Hivyo, sisi tunaenda na wewe na hatutokuacha. Jibu letu utalipata Oktoba kwenye sanduku la kura," alisema Christina Kupaza, mkazi wa Vuga.

Said Dhahabu, mkazi wa kijiji cha Manga Funta, alieleza sababu za kumchagua tena Mbunge huyo kutokana na namna alivyoisaidia jamii yao kutatua tatizo kubwa la maji, ambalo awali lililazimu wananchi hao kutembea umbali wa kilometa nne juu ya mlima ili kufuata maji.

" Ndoa zetu ziliyumba kwa sababu wake zetu walikuwa wanatembea usiku kuchota maji. Lakini baada ya Mbunge wetu kusikia kilio chetu, alituletea rola za maji, sasa tunapata maji ya bomba majumbani mwetu, na wengine wanachota karibu na nyumba zao," alisema Said Dhahabu.

Mariam Mdoe alieleza kuwa changamoto ya maji ilipelekea baadhi ya wasichana kukosa wachumba, kwani wanaume wa mjini walikuwa wakidai hawezi kuwaoa wakati kwao hakuna maji. Hata hivyo, sasa wanapata huduma hiyo kwa urahisi baada ya Mbunge kuwapelekea maji.

Diwani wa Kata ya Funta, Francis Kanju, alisisitiza kuwa kwa yale aliyoyafanya Mbunge huyo, bora yeye asipate udiwani, lakini wamchague tena January Makamba ili aendelee kuwaongoza kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Diwani wa Kata ya Vuga, Jumaa Dhahabu, alifafanua kuwa Mbunge huyo ni kiongozi wa kipekee ambaye anaweza kuwasaidia wananchi wake bila kusubiri serikali.

Aliongeza kuwa katika Kata ya Vuga, Mbunge amefanya mengi ikiwemo kuwajenga shule, zahanati, na kutatua changamoto ya umeme ambapo kila kijiji kimepata umeme, kasoro vitongoji vichache ambavyo tayari ameahidi vitapata umeme. Aidha, aliendelea kusema kwamba miradi mikubwa ya maji imeanzishwa, na wananchi wameshuhudia mabadiliko makubwa baada ya mbunge huyo kuwaongoza

" Mbunge wetu, hata kama hutatokea siku ya uchaguzi, leta shati tu, tutalichagua maana umefanya mengi ambayo hayajawahi kufanywa na Mbunge mwingine aliyepita," alieleza Diwani wa Vuga, ambaye pia ni Mwenyekiti wa kudumu wa Kamati ya Elimu, Afya, na Maji katika Halmashauri ya Bumbuli.

Wananchi wengine kutoka Mgwashi na kata ya Kongoi walieleza kuwa hawana shaka ya kumchagua tena Mbunge wao wakati wa uchaguzi mkuu ujao, kwa kuwa amewafanyia mengi katika sekta zote muhimu. Hata hivyo, walieleza kuwa wanatarajia utatuzi wa changamoto ndogo ndogo zinazohusiana na barabara.

Hassani Kupaza kutoka kata ya Tamota alisisitiza kuwa Mbunge wao anastahili kupata miaka mitano mingine ya uongozi, kwa sababu tangu dunia iumbwe, kijiji chao hakikuwa na umeme wala huduma zingine. Lakini sasa huduma hizi zinapatikana kwa urahisi, ingawa changamoto hazijaisha, wameweza kutatua asilimia kubwa ya matatizo.

Kaimu Meneja wa Wakala wa Mjai vijijini (RUWASA) wilaya ya Lushoto Seleman Mdoe amesema katika Halmashauri ya Bumbuli jumla ya miradi Miwili ya maji yenye thaman ya sh.3.9 billion inaendelea kutekelezwa nakwmaba itakapokamilika jumla ya vijiji 10 vitanufaika.




0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa