Mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe Mussa Kilakala amefanya ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya vyoo vya watumishi,ujenzi wa kinawia mikono pamoja na kichomea taka katika Zahanati ya Kipumbwi.
Hayo yamefanyika leo Julai 10,2024 ambapo amesisitiza matumizi ya mfumo wa usimamizi wa Sekta ya Afya (GoTHOMIS).
Akizungumza mala baada ya ukaguzi wa miundombinu hiyo mhe Mussa Kilakala ameeleza kuwa kwenye matumizi ya GoTHOMIS kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, ni takwa la Serikali na kila Zahanati ihakikishe inatumia mfumo huo.
Ikumbukwe kuwa GoTHOMIS ni mfumo wa kumeneji taarifa na kukusanyia mapato ambao licha ya kuthibiti ukusanyaji wa Mapato lakini pia unasaidia kutunza kumbukumbu za matibabu ya wagonjwa, wanaofika kituoni kupata huduma mbalimbali.
Home »
» DC PANGANI ASISITIZA MATUMIZI YA MFUMO WA GoTHOMIS VITUO VYOTE VYA AFYA.
0 comments:
Post a Comment