Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe Japhari Kubecha Amezindua mafunzo ya Mradi wa E360 wa Uwezeshaji wa Ujasiriamali kwa Wananchi ambao Waliguswa na mradi wa Bomba la Mafuta ,
Mafunzo hayo Yalishirikisha Watu Mbalimbali Wenyeviti wa Mitaa ,Watendaji wa Kata na Mitaa ambao Mradi Huu Umepita , Pia Viongozi wa Dini Pamoja na Wananchi ambao Mradi wa Bomba la Mafuta Uliwagusa ,
Aidha Mkuu wa wilaya Amewaomba washiriki Kupokea mafunzo haya ya Uwezeshaji Kiuchumi na Ujasiriamali ili Waweze Kunufaika na Kuweza Kuwa na Tija kwani Kupitia Mradi Wa Bomba la Mafuta Wameweza kupata Fursa mbalimbali na Kujikwamua Kiuchumi ,
Pia Ametoa Rai kwa Yeyote Yule Kutokwamisha Mradii Huu wa Bomba La Mafuta kwani Ni Mradi Mkubwa sana kwa Nchi yetu na Unatija kubwa sana na Kuendelea kuwasisitiza Wenyeviti wa Mitaa Kutokuwa Kikwazo kwenye Maendeleo ya Mradi na Yeyote Yule ambaye Atakwamisha Serikali ya Wilaya Haitokuwa Tayari Kukubaliana naye .
# TANGA YETU,LANGO LA UCHUMI WA AFRIKA MASHARIKI
0 comments:
Post a Comment