Home » » TANZANIA YA TATU UDUMAVU WA WATOTO AFRIKA

TANZANIA YA TATU UDUMAVU WA WATOTO AFRIKA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
TANZANIA ni nchi ya tatu Afrika inayokabiliwa na tatizo la udumavu wa watoto chini ya miaka mitano unaotokana na ukosefu wa lishe bora.
Hayo yalielezwa na Mkurungezi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Francis Mudaha alipokuwa akitoa mada kwenye mkutano wa ushawishi na utetezi wa uboreshaji masuala ya lishe mkoani hapa uliojumuisha wenyeviti wa halmashauri, wakuu wa wilaya na waganga wakuu wa wilaya zote tisa za mkoa huu.
Alisema utafiti wa mwaka 2010 unaonyesha kwamba Tanzania unapoteza watoto 1,600 kwa mwaka huku watoto watatu wanakufa kila mwezi kwa utapiamlo.
Alisema hali hiyo inasababishia hasara ya zaidi ya sh milioni 815 ya pato la taifa inayopotea kutokana na kuhudumia watoto wenye utapiamlo maeneo mbalimbali nchini.
Mudaha alizitaja athari za utapiamlo kwa watoto kuwa ni kuathiri ubongo, mifumo bora ya kinga za mwili na ukuaji dhaifu ikiwemo uwezo wake wa kufikiri kwa haraka na kuchukua uamuzi.
Hata hivyo aliiomba serikali kuimarisha ulishaji wa watoto wachanga ikiwemo kusisitiza umuhimu wa maziwa ya mama, kuhamasisha uzalishaji wa vyakula mchanganyiko ili kuzuia utapiamlo kwa watoto chini ya miaka mitano.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa, alisema viwango vya utapiamlo kwa watoto chini ya miaka mitano mkoani hapa ni asilimia 49.
Aliahidi kutoa ushirikiano katika kuhamasisha kipaumbele kwenye masuala ya lishe ili kupunguza ukubwa wa tatizo
 Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa