Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kushoto akimkabidhi viatu Mweka Hazina wa timu ya African
Sports,Sad Juma kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Ligi Daraja la pili makabidhiano hayo yalifanyika uwanja wa CCM mkwakwani mjini Tanga
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kushoto akimkabidhi viatu Mweka Hazina wa timu ya African Sports,Sad Juma kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Ligi Daraja la pili makabidhiano hayo yalifanyika uwanja wa CCM mkwakwani mjini Tanga
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akisalimiana na wachezaji wa timu ya Jang'ombe ya Zanzibar ambao wameweka kambi mkoani Tanga wakati alipokwenda kukabidhi vifaa kwa timu ya African Sports.
TIMU
ya African Sports “Wanakimanumanu”imepata msaada wa vifaa vya michezo
kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Ligi daraja la pili itakayoanza
kutimua vumbi.
Vifaa
hivyo ambavyo ni seti ya viatu vilitolewa juzi na Mbunge wa Jimbo la
Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku katika halfa iliyofanyika kwenye viwanja
wa CCM Mkwakwani mjini Tanga
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo,Mbunge Mussa alisema ameamua kutoa
vifaa hivyo ili kuweza kuihamasisha kufanya vizuri katika mashindano
hayo na hatimaye kuweza kurudi ilipotoka.Alisema licha ya timu hiyo kushuka daraja hivi sasa wanapaswa kujiimarisha na kucheza kwa umakini mkubwa ili kuweza kucheza michuano ya ngazi za juu.
“Mimi
ni Mbunge lakini pia ni mwana michezo hivyo nitahakikisha nazisapoti
timu za mkoa huu kwa lengo la kurejea kwenye makali yao ya zamani kwani
michezo ni ajira “Alisema.Nay kwa upande wake,Mweka Hazina wa
timu hiyo,Sad Juma alimshukuru mbunge huyo kwa kutoa vifaa hivyo
ambavyo vitasaidia timu hiyo kuondokana na uhaba uliokuwepo.
“Kama
unavyojua sisi tulikuwa na uhaba wa vifaa vya michezo hususani viatu
na nyenginevyo hivyo alichotupa mbunge tunamshukuru lakini tutakuwa nawe
bega kwa bega “Alisema.Hata hivyo alisema hivi sasa wanaendelea
na maandalizi kwa ajili ya kujiwinda na mashindano hayo wakiwa na
kikosi imara ambacho kimedhamiria kupata mafanikio.
Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
0 comments:
Post a Comment