Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Dkt Juliana Pallangyo akizundua mradi huo
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Dkt Juliana Pallangyo kushoto akipata maelezo ya mradi huo mara baada ya kutembelea kwenye eneo la mtambo huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Mhandisi,Robert Gabriel.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Dkt Juliana Pallangyo akishiriki kucheza ngoma ya wananchi wa Kijiji hicho mara baada ya kuzinduaa mradi huo .
NI ukweli usiopingika utekelezaji wa sekta ya viwanda inahitaji
nishati
ya umeme katika shughuli zake mbalimbali ikiwemo za uzalishaji mali ili
kuweza kupata mafaniko yanayoweza kusaidia kuinua uchumi wao.
Kwani
bila kuwepo kwa nishati hiyo kwa baadhi ya maeneo hasa vijijini kuna
pelekea kushindwa kufikia malengo yao kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa
mbalimbali kwa kuhofia iwapo zitakaa muda mrefu zitaharibika.Licha
ya hivyo lakini pia kukosekana kwa nishati hiyo kuna sababisha
watanzania wenye nia ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo kukwama kufikia
malengo yao waliojiwekea kwa kuvianzisha.
Kufuatia
kuwepo kwa changamoto hiyo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa
Mitaji na Maendeleo (The United Nations Capital Development Fund –UNCDF)
kwa kushirikiana na kampuni ya Ensol Tanzania Limited waliamua
kuanzisha mradi wa umeme wa jua (sola) kwenye kijiji cha Mpale Kata ya
Mpale wilayani Korogwe Mkoani Tanga.
Mradi
huo ambao umekuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Kijiji hicho
umefadhiliwa na Shirika hilo ambao umelenga kuwasaidia kuondokana na
changamoto ambazo zilikuwa zikiwakabili ikiwemo kutumia vibatari wakati
wakienda kujifungua kwenye zahanati ya Kata hiyo.
0 comments:
Post a Comment