Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mchezaji
wa timu ya Bandari Tanga akiruka juu kuwania mpira wakati wa mchezo wa
Mashindano ya Kilimanjaro Cup yanayoendelea kwenye viwanja wa KCMC na
Baptist ambapo mechi hiyo ilikwisha kwa Bandari Tanga kuibuka na ushindi
wa vikapu 64 dhidi ya 57
Wachezaji
wa timu za Bandari Tanga na Baptist wakiwania mpira wakati wa mchezo wa
Mashindano ya Kilimanjaro Cup yanayoendelea kwenye viwanja wa KCMC na
Baptist ambapo mechi hiyo ilikwisha kwa Bandari Tanga kuibuka na ushindi
wa vikapu 64 dhidi ya 57
Kocha
wa timu ya Bandari Tanga Mohamed Fazal akitoa maelekezo kwa timu hiyo
wakati wa mapumzikokulia ni PRO wa Bandari ya Tanga,Moni Jarufu
Kocha
wa timu ya Bandari Tanga,Mohamed Fazal akitoa mawaidha kwa timu hiyo
wakati wa mapumziko kulia ni PRO wa Bandari ya Tanga,Moni Jarufu
Kikosi cha timu ya Mpira wa Kikapu ya Bandari Tanga
TIMU
ya Mpira wa Kikapu ya Bandari Tanga ambayo inashikilia Ubingwa wa
Mashindano ya Kilimanjaro Cup mwaka jana inashiriki tena Mashindano hayo
kutetea ubingwa huo mwaka huu katika mashindano yanayoendelea kwenye
viwanja KCMC mjini Moshi.
Kitendo
cha timu hiyo kuendelea kufanya vizuri katika mashindano hayo kwa mara
nyengine kinaonyesha namna kinavyotumia vema fursa hiyo kuitangaza
Bandari ya Tanga.
Katika
kuhakikisha suala hilo linakwenda kwa vitendo leo timu ya Bandari Tanga
wameibuka na ushindi wa vikapu 64-57 dhidi ya timu ya Baptist katika
mechi iliyokuwa na upinzani mkubwa huku Bandari Tanga ikipambana ili
kuhakikisha inatetea Ubingwa wake na kuondoka na ushindi huo.
Awali
akizungumza wakati akizundua mashindano hayo, Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro, Anna Mgwira amezitaka timu shiriki kutumia fursa ya
mashindano hayo kutangaza utalii wa nchi ikiwemo mlima
Kilimanjaro.“Baada ya mashindano haya timu zote shiriki zitakwenda
kupanda mlima Kilimanjaro ili kuweza kuhamasisha wanamichezo na wananchi
wengine kuweza kutalii mlima huo “Alisema Mkuu huyo wa mkoa.
Mkuu
huyo wa mkoa alitumia nafasi hiyo kuwataka vijana kuchangia damu kwa
wahitaji ambapo katika viwanja hivyo sehemu iliyotengwa kwa ajili ya
kuchangia damu kwa hiari.Mashindano hayo yanaendelea kwa wiki nzima
katika viwanja vya Baptist na KCMC Mkoani Kilimanjaro.
Chanzo Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
0 comments:
Post a Comment