Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wananchi
365 wa kijiji cha Chongoleani watafidiwa shilingi bilioni 3,035 kwa
ajili ya kutoa maeneo yao, ili kupisha ujenzi wa bomba la mafuta
linalojengwa kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Tanga.
Hayo
yamesemwa na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Usimamizi wa Bandari
Tanzania TPATanga, Bibi Janeth Rwuzangi katika mahojiano maalum na
Idara ya Habari (MAELEZO) leo.
Bi Ruzangi amesema kuwa
kwa hapa Chongoleani mradi una ukubwa wa hekta 200 zikiwemo hekta 100
zitakazotumiwa kuweka miundombinu ya mafuta ghafi. Hekta 100 zilizosalia
zitatumika kwa ajili ya shughuli za TPA) kuwekeza miundombinu ya
kupokea mafuta yaliyosafishwa. Vile vile eneo hili limezingatia
maendeleo endelevu ya biashara ya mafuta na gesi katika siku zijazo.
Aliongeza
kuwa TPA itakuwa na wajibu wa kuhudumia meli, kuhakikisha usalama wa
bidhaa, vyombo na watu pamoja na kusimamia masuala ya afya bandarini.
Aidha, Majukumu la TPA yanatarijiwakujikita katika shughuli za
uendeshaji wa majini ikiwemo kuwa na vyombo na boti maalumu kwa ajili ya
kuongozea meli wakati wa kuingia na kutoka kwenye gati la mafuta ghafi.
Akitoa ufafanuzi, Bi Ruzangi amesema vile vile, TPA ina
jukumu la kuhakikisha inahudumia shehena ya vifaa vyote vya ujenzi
katika Bandari ya Tanga kwa kushirikiana na Bandari Kuu ya Dar es
Salaam. Shughuli nyingine ni pamoja na ulinzi wa miundombinu ya majini
pamoja na usalama wa eneo la Bandari ambalo limegawanyika katika sehemu
kuu mbili; ardhini kwenye gati la mafuta na majini kwenye lango la
kuingilia meli na nangani.
Kwa upande wa ajira za TPA
Ruzangi amesemawafanyakazi ambao wataajiriwa ni pamoja na mabaharia,
wahandisi, mafundi, wahasibu, wachumi, watakwimu, vibarua mbalimbali kwa
ajili ya nguvu kazi n.k. Sehemu ya wafanyakazi hawa watatokana na
waliopo sasa kwenye Bandari watakaopangiwa kazi hizo. Hata hivyo TPA
inatarajia kuajiri wengine ambao watalazimika kufanya kazi hizo
kulingana na taratibu za ajira za TPA.
Pamoja na kuwa na
bomba la mafuta, kijiji cha Chongoleani kitafaidika na ujenzi wa
barabara ya kilometa 8 itakayounganisha bandari na barabara kuu ya
Horohoro – Tanga, ambapo kwa kiasi kikubwa itainua uchumi wa wananchi
wanaoishi maeneo hayo kusafirisha mazao, samaki na bidhaa nyingine kwa
urahisi.
Akifafanua uwekaji wa jiwe la msingi Ruzangi
amesemakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe
Magufuli na Mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wanatarajia
kuweka jiwe la msingi la Mradi wa Bomba la Mafuta tarehe 05 Agosti
2017.
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Chongoleani, Bw.
Mbwana Nondo amesema; “Kwa moyo wa dhati kabisa, naomba nimshukuru sana
sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli
kwa kutujali wananchi wake na kutuletea neema ya Mradi wa Bomba la
Mafuta, katika maisha yetu wanachongoleani, hatutaweza kumsahau kwa
kizazi hiki kinachoshuhudia mradi huu na vizazi vijavyo”.
Nondo
alisema kuwa anamuhakikishia Mhe. Rais kuwa kuwa wote watakaopata fursa
kwenye mradi wa Bomba la Mafuta, watafanyakazi kwa bidii ili kujiletea
maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Bomba la
Mafuta la kutoka Hoima Uganda mpaka Tanga Chongoleani lina urefu wa
Kilometa 1445 ambapo kwa upande wa Tanzania itakuwa na jumla ya kilometa
1115 na Uganda 330. Aidha, Mradi utatarajia kusafirisha mapipa laki
mbili na kumi na sita elfu (216,000) kwa siku .
Kijiji
cha Chongoleani ndio kituo cha mwisho ambapo mitambo mikubwa itasimikwa
katika eneo hili kwa ajili ya kusukuma mafuta eneo la baharini ili,
kuweka kwenye vyombo vya usafirishaji kusafirisha maeneo mbalimbali
duniani ambayo Uganda watakuwa wamepata soko.
Tanzania
itafaidika na mradi huu kutokana na kodi, tozo na mrahaba wa bomba la
mafuta, itakayofanywa moja kwa moja na mradi huo. Faida nyingine ambazo,
sio za moja kwa moja ni ajira, fursa za kufanya biashara na uwezekano
wa mikoa 8 ambayo ni Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma,
Morogoro na Tanga.
0 comments:
Post a Comment