Home » » BILL GATES ATUA TANZANIA, ATEMBELEA KIJIJI CHA KICHEBA WILAYANI MUHEZA, TANGA

BILL GATES ATUA TANZANIA, ATEMBELEA KIJIJI CHA KICHEBA WILAYANI MUHEZA, TANGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


William Henry Gates III maarufu kama Bill Gates na Mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft iliyomfanya kuwa mtu tajiri namba moja  duniani na mwanzilishi wa mashirika lukuki yasiyo ya kiserikali yenye kusaidia jamii yupo nchini. Leo ametembelea kijiji cha Kicheba wilayani Muheza katika mkoa wa Tanga kwa lengo la kuangalia maswala mbalimbali ya afya ikiwemo utumiaji wa dawa za mabusha, matende ili kuangalia ni namna gani anaweza kusaidia kwenye sekta hiyo ya Afya.
 Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Mhandisi, Hajat Mwanasha Tumbo (kushoto) akiwa na Bill Gatesbpamoja na mmoja wa viongozi wa kinamama wa wilaya hiyo katika kata ya Kicheba Wilayani humo mkoani Tanga leo
Bill Gates akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa wilaya ya Muheza akiwamo Mkuu wa Wilaya Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Mhandisi, Hajat Mwanasha Tumbo na Mbunge Mhe Adadi Rajabu (wa nne kulia) katika kata ya Kicheba Wilayani humo mkoani Tanga leo
Bill Gates akiwasili na kusalimiana na uongozi wa wilaya ya Muheza katika kata ya Kicheba Wilayani humo mkoani Tanga leo.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa