Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi awasili
mkoani Tanga kutatua migogoro ya ardhi inayoukabili mkoa huo pamoja na
mikoa inayopakana nayo.
Katika
ziara hii Waziri Lukuvi leo amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.
Martin Shigela na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera ili kutatua
migogoro ya mipaka iliopo kati ya Wilaya ya Kiteto Iliyopo Mkoani
Manyara na Wilaya ya Kilindi iliyopo mkoani Tanga ikiwa muendeleo zo wa
mikutano ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro huu ambao umesababisha uvunjifu
wa amani.
Waziri
Lukuvi anatekeleza agizo la Waziri Mkuu Mhe. Khassim Majaliwa ambae
alimuagiza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William
Lukuvi kutatua mgogoro huu uliodumu kwa miaka mingi kati ya Wilaya hizo
mbili pindi alipofanya ziara yake mkoani Tanga.
Ikumbukwe mnamo tarehe 18 Januari, 2017 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifanya ziara
Wilayani Kilindi katika Kijiji cha Mafisa na kuzungumza na wanachi
Kijijini hapo kuhusiana na mgogoro huo na kutoa maagizo kwa viongozi wa
kuchaguliwa kuacha kutumia nafasi zao vibaya kuongoza kwa mihemko au
ushabiki kwa kuwa kufanya hivyo kunapelekea wananchi kufuata ushabiki na
kuvunja sheria zilizopo.
Ili
kutekeleza agizo hili wakuu wa mikoa hii miwili wakiongozwa na Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wamekutana
ikiwa ni muendelezo wa vikao vya kulitafutia ufumbuzi suala hili.
Aidha,
wawakilishi wa wakazi wa kata ya Mnazi wilayani Lushoto na viongozi wa
Halmashauri ya Lushoto walimlalamikia Waziri Lukuvi kuhusu mashamba
matatu ya Mnazi yaliyotelekezwa na mmiliki wa mashamba hayo ajulikanae
kwa jina la Le-Mash Enterprises Limited.
Baada
ya Waziri Lukuvi kusikiliza malalamiko hayo, ameahidi kutembelea
mashamba hayo kesho ili kujionea hali halisi na kuwasikiliza wananchi
ambao wanakabiliwa na mgogoro huu ambao umekuwepo kwa miaka mingi.
0 comments:
Post a Comment