Mtendaji Mkuu Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Prof. Dos Santos Silayo
(kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa Mamlaka ya
Hifadhi za Taifa Tanzania, Ibrahim Mussa (kushoto) alipokuwa akimueleza
mambo mbalimbali ya uhifadhi na changomoto zake inapokuja suala la
kushirikisha vyombo vya habari kabla ya kufungua mkutano wa sita wa
wahariri na wanahabari waandamizi unaohusu sekta ya utalii nchini ambao
umeandaliwa na Hifadhi za Taifa (TANAPA) unaofanyika jijini Tanga 27 -
29, Julai 2017. Pichani kati ni Mkurugenzi Mkuu wa Shrika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA),Allan Kijazi
Katika
mkutano huo Prof Silayo atawasilisha mada "uhifadhi wa misitu ya
hifadhi ya asili na mpango mkakati wa utalii Kesho Ijumaa ya tarehe 28
Julai 2017 saa 05:45 asubuhi na kurushwa moja kwa moja kupitia ukurasa
wa facebook wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania
(www.facebook.com/foresttz).
usikose kuungana naye na atajibu maswali yatakayoibuka kutokana na mada atakayoiwakilisha!
Mratibu wa Mradi wa Misitu ya Hifadhi ya Mazingira Asilia Tanzania, Gerald Kamwenda (Kushoto) akijadiliana jambo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof Dos Santos Silayo mara baada ya kupokea taarifa za wajumbe wa Mkuno Mkuu wa Mwaka wa Wahariri na Wanahabari Waandamizi ulioandaliwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kutembelea Hifadhi ya Misitu Asilia ya Amani Siku ya Jumamosi (Julai 29,2017).

0 comments:
Post a Comment