Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (katikati), akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msasa IBC wilaya ya Muheza mkoani Tanga jana wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo kwa ajili kutatua mgogoro wa hifadhi ya msitu wa Derema. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanaisha Tumbo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (katikati), akimuonesha mwenyekiti wa kamati ya wakulima wa vijiji vitano vya tarafa ya Amani, Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Mohammed Ramadhani Shesha viwango halali vya serikali vya kulipia fidia za mazao kwa wananchi waliondolewa katika eneo la hifadhi ya msitu wa Derema wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo jana kwa ajili ya kutatua migogoro wa hifadhi hiyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanaisha Tumbo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (kulia), akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msasa IBC wilaya ya Muheza mkoani Tanga jana wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo kwa ajili kutatua mgogoro wa hifadhi ya msitu wa Derema.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani, (wa tatu kushoto), akiangalia eneo la Msitu wa hifadhi ya Derema na viongozi wa wilaya ya Muheza Muheza wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo jana kwa ajili ya kutatua mgogoro wa hifadhi hiyo.
Na Hamza Temba - WMU - Muheza, Tanga
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani ameuagiza uongozi
wa Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga kukutana na wakulima 879 wa vijiji
vitano katika Tarafa ya Amani Wilayani humo kwa ajili kufanya uhakiki wa
malipo ya fidia ya mazao waliyolipwa na Serikali ili kupisha eneo la
hifadhi ya msitu wa Derema.
Mhandisi
Makani ametoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika
Kijiji cha Msasa IBC, Tarafa ya Amani, Wilayani Muheza kufuatia
malalamiko ya wananchi hao kupunjwa malipo yao wakati wa ziara yake ya
siku moja wilayani humo kwa ajili kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa
zaidi ya miaka 15 baina Serikali na wananchi wa vijiji hivyo vya
Kisiwani, Kwemdim, Msasa IBC, Antakae na Kambi.
Akisoma
risala ya wakulima hao mbele ya Naibu Waziri Makani, Mwenyekiti wa
Kamati ya wakulima hao, Mohammed Rama Shesha alidai kuwa jumla ya
wakulima 1,128 wa vijiji hivyo wanailalamikia Serikali kwa kuwalipa
viwango pungufu vya malipo ya fidia ya mazao yao tofauti na viwango
vilivyolipwa na Serikali mwaka 2002 kupitia mradi wa FINIDA. Aidha,
alidai kuwa kuna baadhi ya mazao pia hayakulipiwa kabisa fidia hizo.
Akizungumzia
viwango vya fidia hizo Shesha alisema wananchi walilipwa Shilingi
28,800 kwa mche mmoja wa iliki na Shilingi 11,000 kwa mche mmoja wa
mgomba. Alidai viwango hivyo vilibadilika kuanzia mwaka 2005 ambapo
walilipwa Shilingi 3,315 kwa kila mche mmoja badala ya Shilingi 5,100
kama ilivyoainishwa kwenye viwango vya Serikali hivyo akaomba walipwe
kiasi kilichobakia cha shilingi 1,785.
0 comments:
Post a Comment