Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mhasibu Mkuu wa kiwanda cha Nondo cha Unique Steel Rolling Mills kilichopo Tanga, Sikander Omar akizungumza na Wandishi wa Habari waliotembelea kiwanda chake kungalia hali ya uzalishaji
Watendaji wa kiwanda cha Unique Steel Rolling Mills kilichopo Tanga wakiwaonesha waaandishi wa habari sehemu ya kuzalishia Nondo ambayo imesimama kutokana na matatizo ya Umeme
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Mwananchi Boniface Meena akiangalia moja ya Nondo zinazozalishwa na Kiwanda cha Unique Steel Rolling Mills kilichopo Tanga
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Kiwanda cha uzalishaji wa nondo cha Unique Steel Rolling Mills kilichopo Tanga kimesema kimejipanga kufanya uwekezaji mkubwa,Ili kutumia fursa ya uwepo wa ujenzi wa Bomba la gesi kutoka Tanga mpaka Uganda kutumia malighafi kutoka kiwandani hapo.
Hayo yamebainishwa na Mhasibu Mkuu wa kiwanda hicho, Sikander Omar alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari waliotembelea kiwanda hicho Jijini Tanga.Omar amesema kuwa Wakati Serikali ikipambana kuhakikisha viwanda vinakua nchini, baadhi ya viwanda vilivyopo vimekuwa vikikumbana na changamoto mbalimbali zinazozuia uzalishaji kwa wakati."Moja ya changamoto hizo ni kukatika katika kwa umeme bila taarifa jambo linalotia hasara wakati wa uzalishaji.
Mbali na hilo upatikanaji wa mikopo kwa ajili ya kuwekeza zaidi imekuwa ni changamoto kwao,anapambana kukiboresha kiwanda hicho lakini umeme kutokuwa wa uhakika imekuwa changamoto".Amesema Omar.Amesema kwa sasa wanazalisha hadi tani 60 za nondo ambazo nyingi huuzwa mkoa wa Arusha.
Akizungumzia changamoto zilizopo msimamizi wa kiwanda hicho,
Jagjeet Singh alisema umeme unapokatika wakati wa uzalishaji inakuwa ni
hasara kwao kwa kuwa mtambo wa kuyeyusha chuma hupoa na vyuma
vilivyokuwa vinayeyuka ili kutoa nondo huganda.
Kiwanda hicho ambacho kilikuwa cha Serikali na kuzinduliwa Julai 21, 1971 kilisimama na kuanza uzalishaji tena hivi karibuni baada ya kuchukuliwa na mwekezaji huyo. Omar amesema hivi sasa wako katika mchakato wa kutafuta mkopo ili kukiongezea nguvu kiweze kuzalisha zaidi na kutoa huduma katika mikoa zaidi ya Tanga na Arusha ambalo ndilo soko kubwa lao lilipo kwa sasa.
Kiwanda hicho ambacho kilikuwa cha Serikali na kuzinduliwa Julai 21, 1971 kilisimama na kuanza uzalishaji tena hivi karibuni baada ya kuchukuliwa na mwekezaji huyo. Omar amesema hivi sasa wako katika mchakato wa kutafuta mkopo ili kukiongezea nguvu kiweze kuzalisha zaidi na kutoa huduma katika mikoa zaidi ya Tanga na Arusha ambalo ndilo soko kubwa lao lilipo kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment