Home » » CHANELI YA UTALII YA TBC KUZINDULIWA DESEMBA 20 MWAKA HUU

CHANELI YA UTALII YA TBC KUZINDULIWA DESEMBA 20 MWAKA HUU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba akitoa ufafanuzi kuhusu mchakato wa kuanzisha chaneli ya Utalii ndani ya televisheni y Taifa (TBC),mbele ya Wahariri na Waandishi waandamizi mapema jioni ya leo katika katika Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika jana  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba amesema mchakato wa uanzishwaji wa Chaneli ya Habari za Utalii kuzinduliwa Desemba 20 mwaka huu.

akizungumza wakati wa uwasilishaji wa mada ya Chanel ya Utalii kwa Wahariri na Waandishi wa Habari wakati wa mkutano wa Utalii na Tanzania ya Viwanda ulioandaliwa na TANAPA Jijini Tanga..

"Chanel hii ni moja ya vitu ambavyo vitasaidia katika kukuza utalii wetu hivyo sasa tupo katika mchakato na wabia wetu TANAPA, NGORONGORO na wadau wengien wa masuala ya habari" amesema Dr Rioba .

Amesema kuwa kikubwa wanachokiangalia sasa ni aiana gani ya uwekezaji unatakiwa kufanywa hili kufanya chombo hicho kuwa bora zaidi hili kuweza kumvutia kila mtu .

aidha Dk Rioba ametoa fursa kwa wadau na wanahabari kutoa maoni yao juu ya namna gani Chanel hiyo inapaswa kuwa hili kuvutia.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa