Naibu Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) akisikiliza
taarifa ya uwanja alipofanya ziara ya kutembelea uwanja uliyowekewa jiwe la msingi na Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliyopo eneo la Mtaa wa Makoko Ndumi ,Kata ya
Mnyanjani kwa ajili ya kujenga uwanja wa michezo wa kimataifa kwa kushirikiana na FIFA kutoka kwa Mstahiki
Meya wa Jiji la Tanga Mhe.Mustapha Selemani leo Jijini Tanga alipotembelea
alipofanya ziara ya kikazi kufuatilia maendeleo ya shughuli za kisekta Mkoani hapo.
Anitha Jonas- MAELEZO
Tanga
Watendaji wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri watakiwa
kuanzisha Kamati za Michezo
zitakazofanya kazi kwa ukaribu na Baraza La Michezo Taifa (BMT).
Agizo hilo limetolewa
leo jijini Tanga na Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe.Annastazia Wambura alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo
lakutaka kujua maendeleo ya shughuli za kisekta kwa Wizara zinavyotekelezwa
Mkoani hapo na changamoto zake.
“Kamati hizi za Michezo
zitakapoundwa zitasidia kusimamia uendeshwaji wa Michezo katika Mkoa pamoja na
usimamizi wa Vilabu vya Michezo halikadhalika usimamizi wa vyama vya Michezo
kwa kuhakikisha vinakuwa na Katiba pamoja kuzingatia uendeshaji wa shughuli
zake kwa kupitia Katiba hizo ambazo zitatakiwa kuzingatia muongozo”,alisema
Naibu Waziri Mhe.Wambura.
Pamoja na hayo Naibu
Waziri huyo aliwasisitiza kuwa Watendaji wa Mkoa kufanya mchakato wa kupata
Maafisa Michezo waliyotoka katika vyuo vya Michezo vya Serikali kwa lengo la
Maafisa hao kuwa Walimu wa Michezo katika ngazi zote ambapo watasaidia ukuibua wa vipaji vya wanamichezo kuanzia
ngazi ya Kata mpaka Taifa,na kuongeza kipato kwani michezo ni ajira.
Kwa upande wa
Mshahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe.
Mustapha Selemani alimuomba Mheshimiwa Waziri kusaidia kuharakisha ujenzi wa
uwanja wa Kimataifa wa FIFA ambao tayari umeshawekwa jiwe la msingi na
Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) ambapo ujenzi wa kiwanja hicho unatarajiwa
kufanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Naye Msemaji wa Timu
ya African Sports ambaye alikuwa Meya wa Jiji la Tanga Bw.Salim Kisauji alisema
Timu za mpira wa miguu Tanga zimekuwa na changamoto ya ukosefu wa fedha za
uendeshaji na hicho ndiyo chanzo cha kushuka kwa daraja kwa timu hizo katika ligi za taifa.
Pamoja na hayo Naibu
Waziri Wambura alitoa pongezi Mwalimuwa
Mpira wa Basketi Bw. Hemed Rajabu kwa jitihada walizozifanya zakuibua vipaji
vya vijana na kuwasidia vijana 6 kupata nafasi za kusomeshwa Chuo Kikuu bure na
wengine kupata nafasi ya kusomeshwa hata nje ya nchi bure ikiwemo nje pamoja na hao waliyoko katika shule za
sekondari.
Hata hivyo viongozi
wa Timu za soka Mkoa wa Tanga wametakiwa kufanya jitihada za kupata mapato
ikiwemo kuanzisha michezo ya bahati na sibu katika michezo yao kwa lengo la
kupata fedha za kujiendesha.
*************************MWISHO************************
0 comments:
Post a Comment