Home » » Muheza wasikitishwa kifo cha Dk. Kigoda.

Muheza wasikitishwa kifo cha Dk. Kigoda.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdallah Kigoda.
Wakazi wa wilaya ya Muheza, mkoani Tanga, wamesikitishwa na  kifo cha Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdallah Kigoda, ambae atazikwa kesho nyumbani kwake wilayani Handeni, mkoani Tanga.
 
Waziri huyo  ambaye ni mzaliwa wa Handeni alifariki Oktoba 12, mwaka huu nchini India ambako alikuwa amelazwa kwa matibabu.
 
Wilayani Muheza wananchi wengi baada ya kusikia taarifa za kifo hicho, walieleza huzuni na masikitiko yao, wakisema ni mmoja wa mawaziri waliosaidia kuinua uchumi wakati wa utawala wa Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, akiwa Waziri wa Mipingo na Waziri wa Viwanda na Biashara wakati wa utawala wa awamu ya nne unaomaliza muda wake chini ya Rais Jakaya Kikwete.
 
Mkazi wa Masuguru,  Selemani Juma, alisema baada yakupata taarifa msiba huo hakuamini, akisema Dk. Kigoda wakati wa uhai wake alikuwa ni rafiki yake na amekuwa amefanya kazi nzuri katika nafasi alizoshika serikalini.
 
Alisema Dk. Kigoda alikuwa mchapa kazi na alikuwa akitekeleza kwa ufanisi kazi alizokuwa akitumwa katika wizara alizoshika kama waziri.
 
Mkazi wa kitongoji cha Majengo, wilayani hapa, Judi John, alisema Dk. Kigoda alikuwa mmoja wa mawaziri wachapakazi na wanaojituma kutoka mkoa wa Tanga na alisimamia vizuri mkakati wa kuufanya mkoa huo kuwa wa viwanda.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa