Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mgombea
Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi
CCM Dr. John Pombe Magufuli akihutubia kwenye mkutano wa kampeni
uliofanyika kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga leo, Dr. Magufuli
amewaomba wananchi wa Tanga kumpigia kura za ndiyo ili aweze kufanya
kazi na kulitumikia taifa yeye kwake ni Kazi tu kwani hata biblia
inasema asiyefanya kazi na asile,
Uchaguzi
Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unatarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba
Mwaka huu nchini kote ukishirikisha vyama mbalimbali vya kisiasa.(PICHA
NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-TANGA)
Mgombea
Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi
CCM Dr. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akihutubia kwenye
mkutano wa kampeni zake uliofanyika kwenye viwanja vya Tangamano mjini
Tanga.
Mwanamuziki nguli hapa nchini Diamond Platnumz akifanya vitu vyake jukwaani katika mkutano wa kampeni.
Mwanamuziki Ali Kiba akionyesha uwezo wake katika jukwaa wakati akitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni wa CCM jijini Tanga.
Mzee
Yusuf Makamba akizungumza neno katika mkutano huo na kuwafunda wananchi
wa mkoa huo kutopotenza kura yao na kumpa Dr. John Pombe Magufuli wa
CCM ili awatumikie.
Tangamano ikiwa imetapika umati wa wananchi wakimsikiliza Dr. John Pombe Magufuli.
Yamoto Band wakitifua jukwaa.
Mwanamuziki wa muziki wa taarab Mzee Yusuf naye akipagawisha wananchi katika mkutano huo.
Kada
wa CCM na mwenyekiti wa Chama cha walemavu Ndugu Amon Mpanju
akiwahutubia wananchi na kumpigia debe Mgombea Urais wa jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe
Maguful.
Ummy Mwalimu akizunguza jambo katika mkutano huo.
Mwigulu Nchemba naye akatema cheche na kusema wapinzani ni watu wa dili tu, kila kitu dili.
Mgombea
Ubunge jimbo la Bumbuli akimkaribisha Mgombea Urais wa jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe
Magufuli mkoani Tanga.
Mgombea
Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi
CCM Dr. John Pombe Magufuli akiwapungia mikono wananchi wa mkoa wa Tanga
mara baada ya mkutano kumalizika.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Ndugu Abdallah Bulembo akizungumza na
mgombea ubunge wa jimbo la Bumbuli Mh. Januari Makamba kulia ni Mgombea
ubunge wa jimbo la Iramba Magharibi.
Mgombea
Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi
CCM Dr. John Pombe Magufuli akihutubia kwenye mkutano wa kampeni
uliofanyika mjini Pangani leo.
Baadhi
ya vijana waliokuja kumsikiliza Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya
Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli
wakifuatilia hotuba yake huku wakiwa juu ya miti.
Akina
mama wakiwa wamejifunika na mabango yenye ujumbe wa kampeni ya Mgombea
Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM
Dr. John Pombe Magufuli yanayosema Magufuli Hapa Kazi Tu wakiwa katika
mkutano wa kampeni mjini Pangani.
Vijana
wakiwa katika miti wakimsikiliza Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano
ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli
wakati akiwahutubia wananchi.
Hapa ni rangi za CCM tu.
Hii
nyumba iliyopo kijiji cha Mkuza Mheza ni full mchanganyiko wao hawana
bifu wanadhihirisha kwamba siasa siyo uadui kwa kuweka picha za wagombea
wa CCM na UKAWA.
Mzee huyu na Mgombea Udiwani wake kata ya Mkuza.
Hawa
wanaonekana wamekunwa na sera za Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano
ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli
Hapa wakapaza zaidi sauti zao wakisema we Tingatinga letuuu!!
Mgombea
Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi
CCM Dr. John Pombe Magufuli akimnadi Balozi Adadi Rajabu ambaye
anagombea ubunge kupitia jimbo la Muheza.
Mgombea
Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi
CCM Dr. John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa kampeni mjini Muheza.
Mgombea
Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi
CCM Dr. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Balozi Adadi Rajabu
mgombea ubunge wa jimbo la Muheza.
Mchezea Chatu wa ngoma za utamaduni naye hakusita kufanya mambo yake katika mkutano wa kampeni wa CCM mjini Muheza.
Vijana wa Kabuku wakampokea Dr. John Pombe Magufuli.
Mgombea
Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi
CCM Dr. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mkata akiwa
njiani kwenda Muheza, Pangani na Tanza mjini kwa ajili ya mikutano ya
Kampeni ambapo aliwaambia atahakikisha anatatua tatizo la maji mkata
mara atakapochaguliwakuongoza nchi ya Tanzania.
Wananchi
wakimsikiliza Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia
Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli huku kukiwa na madumu
kwa ajili ya kuchotea maji Mkata ina tatizo kubwa la maji safi ya
kunywa.
0 comments:
Post a Comment