Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAKATI Taifa likiwa katika mikakati ya kuzuia ugonjwa hatari wa Ebola, jopo la wataalamu wa afya kutoka Wilaya nane za Mkoa wa Tanga limekutana ili kupeana elimu dhidi ya ugonjwa huo.
Wataalam hao kutoka hospitali za umma na binafsi wamekutana ukumbi wa mikutano katika hospitali ya Mkoa Bombo, kwa lengo la kupeana elimu jinsi ya kumhudumia mgonjwa wa Ebola sanjari na kuzitambua dalili za ugonjwa huo, athari, kujikinga na kujua mpango mkakati wa kimkoa.
Akitoa elimu kwa wataalamu hao, Ofisa Afya na Majanga Mkoa wa Tanga, Dk. Jumanne Magoma, aliwatahadharisha watanzanzia kujiepusha na ugonjwa huo hatari usio na tiba, ambako tayari umesababisha vifo vya watu katika nchi za Afrika Magharibi.
Awali, akifafanua umuhimu wa kushiriki hospitali za watu binafsi, Mkurugenzi wa hospitali za binafsi, Samwel Ogillo, aliwaasa watanzania kubadilisha tabia na kuepukana na mila na desturi za makabila, ambazo zinaweza kuwa chanzo cha maambukizi ya ugonjwa huo.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk. Asha Mahita, alisema Mkoa wake umejipanga vema kukabiliana na janga hilo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu mijini na vijijini.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego, aliwataka madaktari hao kujiandaa kikamilifu kuhakikisha gonjwa hilo halipenyi katika mipaka ya Tanzania.
Wakizungumza na Tanzania Daima, baadhi ya wahudumu akiwemo Happynes Digson na Jucetis Mwambashi, waliufananisha ugonjwa huo kuwa ni sawa na vita, hivyo hawana budi kujiandaa kikamilifu kwa kuvaa silaha zote za maangamizi ambazo wanazipata kupitia semina hizo elekezi.
Tayari Mkoa wa Tanga umetenga eneo maalumu kwenye hospitali ya Wilaya ya Mass Shamba, ikiwa ni maandalizi ya kukabiliana na ugonjwa huo kama
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment