Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
JESHI la Kujenga Taifa (JKT), limewataka wahitimu wa mafunzo ya
awali kuzingatia utii na uwajibikaji katika jamii wanazoishi ili
kuepuka migogoro.
Aidha, kupitia mafunzo waliyoyapata yasiwe kwa faida yao pekee bali kwa jamii nzima.
Wito huo umetolewa jana na Kanali Ferix Samillan, wakati wa ufungaji
wa awali wa kundi la tatu la miaka 50 ya JKT kwa vijana waliomaliza
kidato cha sita.
Kanali Samillan, alisema kuwa ni jukumu lao kuwalea vijana wa
kitanzania, na kwamba vijana hao wamemaliza mafunzo yao ya awali
takribani miezi mitatu, hivyo wako tayari kulitumikia Taifa lao huku
wakiwa na uadilifu.
“Pia nawaasa kutokujiingiza katika makundi ambayo yanataka kuigawa
nchi yetu, zingatieni uzalendo… Tanzania ni nchi yetu na hakuna ambaye
ataipenda zaidi ya sisi wenyewe,” alisema KanaliSamillan.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo, ameitaka serikali
kuandaa mpango maalumu kwa vijana hao ambao wamemaliza mafunzo, kwa
kuwaandalia kitu ambacho kitawasaidia katika maisha yao baada ya
kuhitimu.
Alisema kupitia mafunzo hayo, vijana hao watakuwa ni wa kipekee
katika jamii zao hasa kwa wale wanaoona mafunzo haya hayana maana,
kwani mtaani kuna maneno sana juu ya jambo hili.v
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment