Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mchuuzi wa matango katika eneo la Chekereni Wilaya ya Moshi Mkoa wa
Kilimanjaro akitafuta wateja wa matunda hayo jana, ambapo alikuwa akiuza
Sh1,000 kwa fungu moja lililopo kwenye bakuli
Wakulima wa matunda na mbogamboga wilayani hapa, wameiomba
Serikali itekeleze ahadi yake ya kuwajengea kiwanda cha kusindika
matunda ili wajihakikishie soko la uhakika.
Wakizungumza katika Kongamano la Machungwa na
Matunda lililofanyika juzi, wakulima hao walisema kutokana na kukosekana
kwa soko la uhakika, mazao yao huozea shambani na hivyo kujikuta
wakiingia hasara kubwa.
Walisema hata wapatapo soko kutoka kwa wafanyabiashara wanaowafuata vijijini, hulazimika kuyauza kwa bei ya hasara.
“Sisi wakulima wa machungwa na mbogamboga tutazidi
kuwa maskini na tutaendelea kuwatajirisha wenye fedha. Tukivuna
machungwa tukakaa nayo ndani zaidi ya siku tatu au nne huoza, hivyo
tunalazimika kuyauza kwa bei ya kutupa ili mradi tuambulie hata fedha
kidogo,” alisema Jumanne Mhina, mkazi wa Mkwaja.
Hata hivyo, Wakulima hao walihoji tatizo
linalokwamisha kujengwa kwa kiwanda hicho ambacho waliahidiwa muda mrefu
na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Mwenyekiti wa wakulima wa machungwa, Fikirini Juma
alisema tatizo hilo linawafanya kwa sasa waendeshe kilimo hicho kama
sehemu ya bustani badala ya zao la biashara kutokana na kutokuwa na
faida nalo.
Alisema mbali ya kukosekana kwa soko, pia barabara ni tatizo jingine linalochangia mazao yao kuharibika
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment