Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
HUKUMU ya kesi namba 38/2013 inayomkabili Mweka Hazina wa
Kinondoni, Alfred Mlowe na wenzake 12 iliyotarajiwa kutolewa jana
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tanga, imeahirishwa hadi Julai
24 mwaka huu baada ya mmoja wa watuhumiwa kushindwa kufika mahakamani.
Kabla ya kuahirishwa kwa hukumu ya kesi hiyo, Hakimu Maira Kasonde
alibaini kutokuwapo mahakamani kwa mtuhumiwa Allen Meena na kumtaka
mdhamini aeleze sababu ya mtuhumiwa huyo kutokuwapo mahakamani.
Mdhamini wa Meena, alimueleza Hakimu Kasonde kuwa mtuhumiwa huyo
ameshindwa kufika mahakamani kutokana na kusumbuliwa na presha na
malaria.
Kutokana na hali hiyo, Hakimu Kasonde alimtaka mdhamini huyo
kuhakikisha tarehe nyingine itakayopangwa mtuhumiwa anahudhuria
mahakamani.
Watuhumiwa wengine katika kesi hiyo ni Rickson Lema, Rehema Kajembe,
Lusungu Masangula, Dk. Clement Shembilu, Alfa Moshi, Ally Mkongelwa,
Halima Kaima, Ahmad Shemu, Ramadhani Mzonge na Primi Mamseri.
Watuhumiwa hao wanadaiwa kati ya Desemba Mosi na 29, mwaka juzi
walitumia madaraka yao vibaya na kumpatia kazi ya ujenzi wa barabara ya
Raskazoni, Mkandarasi Y.N Investment ambaye hakuwa na sifa.
Upande wa mlalamikaji ambao ni Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (Takukuru) walidai utoaji wa zabuni kwa kampuni hiyo ilikuwa ni
kinyume na kifungu 80(5) cha kanuni ya manunuzi ya umma kutokana na
zabuni kutangazwa mara moja.
Katika utetezi wao, washitakiwa hao wakiongozwa na wakili wao, Mwita
Waissaka, walikana kutoa zabuni hiyo kinyume cha taratibu.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment