Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Dr. F. Ngundulile Mbunge wa Kigamboni akisistiza Jambo katika uzinduzi wa Solar.

Dr. Faustine Ndugulile Mbunge wa Kigambon, 1 left. Dilesh Solank Mkurugezi Steps Solar mwenye miwani.

King Majuto.

Jacob Stephen akiongea na wananchi Mjimwema.

King Majuto na Nisha.
---
Mwigizaji mkongwe katika
tasnia ya filamu Amri Athuman ‘King Majuto’ wiki iliyopita akiwa kama Balozi wa
Steps Solar alitoa msaada wa kukifungukia Solar kituo cha Polisi cha Mjimwema,
ikiwa katika kampeni za kuhakikisha kila mtanzania anafaidika na matumizi ya
nishati ya umeme Nuru.
Akiongea na Waandishi wa habari
katika hafla iliyoandaliwa na kampuni ya Steps Entertainment ambao ndio wafadhali
wa msanii huyo, alisema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikisambaza filamu zake lakini
kuna utaratibu wa kutoa misaada kwa jamii, kwake yeye ameona tatizo
linalowakabili watu wengi nje ya miji ni umeme.
“Nimeanza kampeni kama Balozi
wa Steps Solar kuwasaidia wapenzi wa kazi zangu, ambazo ninaamini bila wao
siwezi kabisa kuwa King, kama vile mnavyopenda kuniita, nimeanza katika kituo
cha Polisi cha Mjimwema lakini nikiwa na wenzangu tutafika sehemu nyingi zaidi,”alisema
King Majuto.
Afisa mahusiano wa kampuni
hiyo Moses Mwanyilu amesema kuwa mradi huo ni endelevu ambapo wanatarajia
kufunga Steps Solar katika vituo vya Kituo cha Yatima Tuangoma, Mjimwema, vituo
vya Polisi ni Mjimwema na Ferry, vituo
vya afya ni Mjimwema, Ungindoni, Homboza Chanika na Tuangoma.
Msanii huyo aliambatana na
wasanii wengine ambao pia ni mabalozi wa Steps Solar, ambao ni Jacob Stephen ‘JB’
na Salma Jabu ‘Nisha’ mgeni wa heshima katika hafla hizo alikuwa Mh. Dr.
Faustine Ndugulile mbunge wa Kigamboni.
0 comments:
Post a Comment