Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MWANDISHI wa habari wa Kampuni ya New Habari Cooperation Mkoa wa
Tanga, Oscar Assenga, ameteuliwa kuwa msemaji mpya wa klabu ya Coastal
Union ‘Wagosi wa Kaya’ yenye makazi yake barabara ya 11 jijini hapa.
Uteuzi huo umefanywa katika kikao cha Kamati ya Utendaji kilichoketi
juzi na kupendekeza mwandishi huyo kuwa msemaji, ambaye atakuwa na
jukumu la kuhakikisha klabu hiyo inatangazwa ipasavyo kwa mujibu wa
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Awali nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Hafidh Kido, ambaye alibwaga manyanga hivi karibuni.
Akizungumza jijini hapa jana, Katibu wa Coastal Union, Kassim El
Siagi, alisema waliamua kumteua mwandishi huyo kutokana na uwajibikaji
wake na kuwa mstari wa mbele kuandika habari zinazochochea maendeleo ya
michezo kwa Mkoa wa Tanga kwa ujumla.
El Siagi alisema pia waliamua kufanya hivyo, kwa sababu ni mkazi wa
jijini Tanga ambaye anaweza kutumia nafasi yake vizuri kwa ajili ya
kutoa taarifa mbalimbali za timu hiyo kwenye vyombo husika na kwa
wakati.
Katika hatua nyingine, El Siagi alisema klabu hiyo inaendelea na
mchakato wa kuhakikisha inasajili wachezaji mahiri, ambao wataweza
kuhimili mikikimikiki ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu ujao.
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment