Home » » TANGA WAHOFIA KUWA KIZANI

TANGA WAHOFIA KUWA KIZANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Baadhi ya kampuni na wamiliki wa viwanda mkoani Tanga, wameingiwa na hofu ya kupungua kwa kasi ya uzalishaji wa bidhaa za viwandani, kufuatia kutokuwepo umeme wa uhakika na ukataji holela wa huduma hiyo.
Hayo yalielezwa jana katika kongamano la wadau wa watumiaji wa umeme Kanda ya Kaskazini, lililofanyika mjini hapa na kuelezwa kuwa, ili kuwavuta wawekezaji wa ndani na nje, Serikali ilipatie ufumbuzi tatizo la umeme.
Walisema kutokuwepo kwa umeme wa uhakika ni chanzo cha uzalishaji mdogo wa bidhaa viwandani, jambo linalochangia kupunguza wafanyakazi wa viwandani.
Ilielezwa Serikali imekuwa ikikosa mapato kutokana na wawekezaji kushindwa kuzalisha bidhaa.
 Chanzo:Mwananchi

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa