Halmashauri ya jijini hapa imetakiwa
kushirikisha wananchi pamoja na sekta binafsi katika miradi ya maendeleo
ili kuleta matokeo bora na ya haraka pamoja na kuchochea kasi ya
mabadiliko ya kiuchumi.
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,
Chiku Gallawa wakati wa ziara yake katika Kata ya Kati(Central)
iliyokuwa na lengo la kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye
kata hiyo.
Alisema, halmashauri hiyo bila ya kushirikisha
wadau hasa wa sekta binafsi haitaweza peke yake kutoa huduma sambamba
na kuleta maendeleo na mabadiliko kwenye shughuli mbalimbali hasa za
kijamii.
“Halmashauri ya Jiji la Tanga tuache umangimeza
kwa kutaka kila kitu tufanye wenyewe, ni lazima ifike mahali mtoe nafasi
kwa sekta binafsi kuwasaidi katika shughuli za kimamendeleo na nyie
mbakie kwenye ukaguzi pekee,”alisema Gallawa.
Aliongeza kuwa halmashauri ndiyo yenye wajibu wa
kuandaa mazingira ya ajira katika ngazi zote kuanzia kwenye mitaa hadi
Jiji na kuwashauri waandae mazingira ya ajira kwa vijana badala ya
kung’ang’ania kila jambo.
Akizungumzia suala la usafi wa jiji , Gallawa
aliwashauri kuwaachia vijana kazi hiyo ili waweze kujiajiri na
halmashauri wabaki na jukumu la kusimamia pamoja na kukagua.
Awali Ofisa Usafishaji wa Jiji, Sylvester Magobo
akitoa taarifa ya hali ya usafi, alisema jiji linakadiriwa kuzalisha
wastani wa tani 240 za taka ngumu kila siku na kuhifadhiwa kwenye maeneo
ya uzalishaji kwa hivi sasa.
Alisema wanakabiliwa na changamoto za upungufu wa
vifaa vya mifumo ya uendeshaji ambapo uboreshaji wake utawezesha maeneo
yote kupata huduma yenye mitiririko imara na wa haraka.
“Uwezo wa jiji ni kukusanya taka kwa kiwango cha
asilimia 84 ya taka zinazozalishwa katika kata 14 za mjini hapa,hivyo
bado tunakabiliwa na upungufu wa vifaa vya kuzolea vilivyo na
ubora,”alisema na kuahidi kujipanga vyema.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment