Ngalawa zikiwa katika mstari kwa ajili ya kuanza mashindano
katika pwani ya Kijiji cha Kigombe wilayani Muheza.
Meneja mauzo wa ZANTELTanzania Salum Ngururu, akikamkabidhi zawadi mshindi wa kwanza katika
mashindano ya Ngalawa, Juma Mgeni zawadi yake.
Sehemu ya umati wa wananchi
wakifuatilia michuano ya Ngalawa.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF),
kizindua mashindano ya Ngalawa Wilayani Muheza.
Mashindano ya Ngalawa yafana Tanga
Na Mwandishi Wetu, Muheza.
Mashindano ya ngalawa yaliyofanyika jana
Wilayani Muheza katika Kijiji cha Kigombe yamefana huku Kampuni ya simu ya
ZANTEL ikifanikisha kwa kutoa zawadi .
Kutokana na hali hiyo Mbunge wa Viti Maalum
Amina Mwidau (CUF), ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo amewataka
vijana washiriki katika michezo badala ya kukaa vijiweni.
Kauli hiyo aliitoja wakati akifungua mashindano ya kwanza ya
Ngalawa mkoani Tanga yaliyofanyika kwenye Pwani ya Kijiji cha Kigombe wilayani
Muheza.
Mwidau alisema kupitia michezo vijana wataweza kupata fursa nyingi
ikiwemo elimu na ujunzi kutoka kwa wenzao ,burudani pamoja na kujenga afya za
kimwili na kiakili.
“Mahindano haya ya Ngalawa hapo awali yalikuwa yanafanyika ngazi ya
kijiji lakini kupitia kwa wadhamini Kampuni ya simu ya ZANTEL tumeweza
kuyafanya kimkoa kwa lengo la kuibua fursa za ajira kwa vijana na kwashirikisha
watu katika michezo, ”alisema Mwidau.
Nae Meneja mauzo wa ZANTELTanzania Salum
Ngururu, alisema kuwa lengo la kudhamini mashindano hayo ni
kurudisha faida wanayopata kwa jamii kutoka na huduma zake na kuendelea
kuwatambulisha bidhaa zinazotolewa na kampuni hiyo.
Alisema ZANTEL itakuwa ikiboresha zawadi za mashindano hayo kila mwaka ili
yaweze kuvuta washiriki wengi. Mshindi wa kwanza alijipatia kitita cha Shilingi
laki tatu, kikombe cha ushindi pamoja na medali za dhahabu. Katika mashindano
hayo mshindi wa kwanza aliibuka ambaye aliweza kujinyakuliwa zawadi hiyo.
Mashindano hayo yalishirikisha jumla ya Ngalawa thelathini zilizokuwa na
washiriki watano ambapo washiriki walitoka katika Wilaya za Tanga, Pangani na
Muheza huku Wilaya ya Mkinga ikishindwa kushiriki kutokana na kushindwa kufanya
maandalizi mazuri.
0 comments:
Post a Comment