Home »
» TRA waaswa kutoa huduma bora
TRA waaswa kutoa huduma bora
|
|
MAMLAKA ya Mapato (TRA) imetakiwa kutoa huduma bora ili
kuwafanya walipa kodi walipe kwa hiari, hivyo kuongeza pato la serikali
na kukuza uchumi wa taifa.
Imeelezwa kuwa elimu wanayotoa kwa walipa kodi ni muhimu, hivyo
inatakiwa kutolewa mara kwa mara na kuongeza kuwa uelewa wa mlipa kodi
juu ya sheria na taratibu za kodi wanazolipa utawafanya walipe kodi
zao kwa hiari.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego
alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa maadhimisho ya saba ya Siku ya
Mlipa Kodi yaliyofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo, mjini
hapa.
Dendego alisema mamlaka hiyo inatakiwa kutoa huduma bora kwa walipa
kodi na wananchi wa Tanzania kwa lengo la kukusanya mapato ya serikali
kwa kiwango kikubwa.
Kwa upande wake, Meneja wa TRA mkoani hapa, Nyonge Mahanyu, alisema
wanatumia siku hiyo kuwakumbusha wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiari,
kwa wakati na kutoa risiti.
Awali katika uzinduzi huo mkoani Tanga imetoa msaada wa shuka 100
katika Hospitali ya Bombo, zenye thamani ya sh milioni 1.6.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Mganga Mfawidhi wa
hospitali hiyo, Dk. Jumanne Karia, alitoa wito kwa wanaotaka kutoa
misaada wawashirikishe ili waweze kueleza hitaji lao, kwani hospitali
ya mkoa huo ina ukosefu wa vifaa vingi.
Chanzo;Tanzania Daima
|
|
0 comments:
Post a Comment