Na Yusuph Mussa, Lushoto
Walimu watano kwenye Halmashauri
ya Bumbuli wilayani Lushoto mkoani Tanga wanalipwa mishahara wakiwa wametoroka
eneo la kazi, huku wengine wakienda kusoma bila kumuaga muajiri wao
Akizungumza kwenye Baraza la Madiwani juzi
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,Patricia Mbigili aliwataja walimu
hao watoro kuwa ni William Kilapilo, Wilbert Mbwambo, Juma Vumba, Ali Mwehuti,
Abeli Mkope na Ramadhan Mwande.
"Kilapilo ametoroka tangu 2011, Mbwambo
2012 na Vumba 2012, hawa wote wanafundisha Shule ya Msingi Kwemkomole. Wengine
ni Mwehuti 2012 na Mkope 2012 Shule ya Msingi Kwamhe na Mwande wa Shule ya
Msingi Kwediwa ametoroka mwaka 2011.
"Walimu hawa wametoroka eneo la kazi na
kwenda kusoma bila utaratibu, lakini tutazingatia maazimio yenu madiwani kuwa
tusimamishe mishahara ya walimu hao mara moja," alisema Mbigili ambaye pia
ni Ofisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Bumbuli.
Diwani wa Kata ya Milingano, Ramadhan
Hozza ambaye ni mmoja wa walioathirika kwa kutorokwa na walimu alisema elimu ya
Tanzania inashuka kwa mambo mengi kwa vile baadhi ya walimu wanatumia ngazi ya
kuajiriwa kama sehemu ya wao kwenda kusoma, lakini si kufundisha watoto wao.
Diwani
wa Kata ya Vuga alisema, baadhi ya walimu hawakai kwenye vijiji vyenye shule
wanazofundisha, bali mjini, matokeo yake inabidi wapangiwe ratiba ya kuanza
kufundisha saa nne kwa vile wanafika wakiwa wamechelewa..
Chanzo: Majira
0 comments:
Post a Comment