5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mazoezi Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga jana.
1
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akivishwa vazi la asili la kabila la Wadigo, na Mwenyekiti wa Umoja wa Wazee wa Wilaya ya Korogwe, Abdallah Semkiwa, wakati wa sherehe za kilele cha Siku ya Wazee Duniani, zilizofanyika mkoani Tanga.
01
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Wazee waliohudhuria katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani, baada ya kuhutubia katika sherehe hizo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Mandu, Korogwe Mkoani Tanga jana Okt. 01, 2013. (Picha na OMR).
03