MKUU wa Mkoa (RC) wa
Tanga, Luteni mstaafu Chiku Gallawa, amewataka wakazi wa Jiji la Tanga na
maeneo ya jirani kuchangamkia ajira zinazotolewa na Kiwanda cha Saruji cha
Rhino kilichopo katika Kata ya Maweni jijini hapa.
Gallawa alitoa
ushauri huo baada ya kutembelea eneo la kiwanda hicho na kushuhudia ujenzi
unaoendelea, ambapo alielezwa kuwa itakapofika Julai mwakani kiwanda hicho
kitakuwa kimeanza uzalishaji.
Mkuu huyo wa mkoa
alielezea lengo la kufanya ziara yake kiwandani hapo ni kutaka kujua changamoto
zinazokikabili kiwanda hicho alichoeleza kuwa kitakapokamilika kitakuwa
kimepunguza tatizo la ajira kwa wananachi.
“Ndugu zangu sisi
kama mkoa tunataka mmalize haraka ujenzi wa kiwanda hiki ambacho kitakuwa
chachu ya maendeleo ya ajira mkoani hapa na taifa kwa ujumla,” alisema Gallawa.
Kwa upande wake mmoja
wa wamiliki wa kiwanda hicho, Sudheer Khaqram, alisema kiwanda hicho
kitakapokamilika watakuwa wamekwisha kuajiri watu wa jinsia zote kutokana na
mchakato wa kutoa ajira unaoendelea kiwandani hapo kwa sasa.
“Tunatarajia kuwa na
wafanyakazi 300, kwa sasa waliopo ni 100, ni fursa nyingine ya ajira kwa wakazi
wa Tanga na maeneo ya jirani,” alisema Khaqram.
Chanzo: Tanzania
Daima
0 comments:
Post a Comment