MKUU wa Mkoa wa Tanga, Luteni Mstaafu Chiku Gallawa
amewaonya askari wa kitengo cha usalama barabarani kuacha tabia ya kupokea
rushwa kutokana na makosa yanayofanywa na madereva kwani kufanya hivyo ni
kulidhalilisha Jeshi la Polisi.
Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa mgeni rasmi
katika uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama, iliyofanyika kimkoa katika
viwanja vya Tangamano, jijini Tanga na kitaifa mkoani Mwanza.
Gallawa alisema baadhi ya trafiki ambao sio
waaminifu, wamekuwa wakiwaomba rushwa wanapokuwa barabarani na matokeo yake
wanadhalilisha jeshi kwa kulipaka matope hivyo ni vema kuacha tabia hiyo.
Hata hivyo, ameitaka Halmashauri ya Jiji la Tanga
kukarabati miundombinu ya barabara ili kupunguza ajali zisizo za lazima kwa
wananchi.
Mbali na hayo, pia amewataka wananchi kuwafichua
watu wanaoiba miundombinu ya barabara kwa kuifanya vyuma chakavu matokeo yake
ajali zinazidi kuongezeka.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment