Majanga ya ukata yanayowakumba wasanii wengi wanaochipukia
katika muziki wa kizazi kipya na hivyo kushindwa kuingia studio kurekodi nyimbo
zao yamepata mkombozi baada ya studio ya Gangstar records ya jijini Tanga kutangaza
kurekodi nyimbo za wasanii hao bure.
Producer Dan (kushoto) akiwa na mwandishi wa habari Dotto Kahindi
Producer wa studio hiyo Dan amesema wameamua
kufanya hivyo ili kutoa fursa kwa wasanii wenye vipaji kurekodi nyimbo zao na
hivyo kuonyesha vipaji vyao kwa jamii.
Mkoa wa Tanga ni miongoni mwa mikoa michache yenye wasanii
wenye vipaji imefanikiwa kutoa wanamuziki kama akina Matonya, Suma Lee, C pwaa,
Mkoloni, TNG, Roma mkatoliki, na wengine kibao.
Hawa ni wale ambao wamefanikiwa kutoka na kutambulika katika
maeneo mengine nje ya mkoa huo, lakini kuna msululu mrefu wa wasanii tena wenye
vipaji ambao hawajapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kutokana na kukosa
sapoti ya kuingia studio lakini sasa wameipata nafasi hiyo.
Cosh Cash
Tutegemee kupata vipaji vipya kutoka Tanga 2013
Robby Kiss
Babylon
0 comments:
Post a Comment