CHAMA cha Walimu (CWT), Mkoa wa Tanga, kimetoa msimamo wake juu ya
mgogoro wa hivi karibuni kati ya walimu wa Shule ya Sekondari Kiomoni na
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego. Akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake jana, Katibu wa chama hicho mkoani hapa, Ndelamio
Mangesho, alisema ofisi yake ilipokea malalamiko kutoka kwa walimu wa
shule hiyo, kuwa mkuu huyo wa wilaya anataka kuwafukuza katika nyumba za
shule hiyo.
Alisema kwamba, kauli ya mkuu huyo wa wilaya kutaka majengo hayo yatumike kama kituo cha afya, iliwashitua walimu na kujihisi wao hawafai kuishi katika nyumba hizo zilizokuwa mali ya Kampuni ya Sinohaidro, iliyokuwa ikijenga Barabara ya Tanga Horohoro.
“Msimamo wetu juu ya majengo haya ni kutaka yatumike kwa kazi za elimu kama yanavyotumika sasa na pasijengwe miundombinu mingine, kwani eneo lenyewe ni mali ya shule hivyo ni busara walimu wakaendelea kuyatumia,” alisema Ndelamio.
Alizitaja sababu za kutotaka majengo hayo yatumiwe kwa matumizi mengine, kuwa unaweza ukazuka mgogoro katika eneo hilo zitakuwapo taasisi mbili zenye kazi tofauti.
“Sababu nyingine ni kwamba, wakati majengo haya yanachukuliwa kutoka kampuni hiyo, kulikuwa na mkataba kati ya Halmashauri ya Jiji la Tanga na kampuni husika ambao unaelekeza, kwamba shule ndiyo inayopaswa kumiliki majengo hayo kwa kuwa yako katika eneo la shule.
“Kwenye mkataba inaonekana wadau wengi walishirikishwa na pia waliridhia eneo hilo kuwa walimu waishi pale,” alisema Mangesho.
Awali walimu wa shule hiyo walilalamika kupitia vyombo vya habari, kuwa mkuu wa wilaya ametoa kauli ya kuwataka waondoke katika majengo hayo na kwamba yanatakiwa kutumika kama kituo cha afya.\
CHANZO MTANZANIA

0 comments:
Post a Comment