Home » » HALI MBAYA SHULE ZA MSINGI.. WIZARA HUSIKA WANALIONA HILI? SHUHUDIA

HALI MBAYA SHULE ZA MSINGI.. WIZARA HUSIKA WANALIONA HILI? SHUHUDIA



 Nyumba ya mwalimu
inapotumika kama darasa.Kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa Shule ya
Msingi Rwengera Darajani Wilaya ya Korogwe imeamua kutumia nyumba hii ya
mwalimu kama darasa la awali kwa muda.
 Hili ni moja
ya darasa la Shule ya Msingi Kitopeni Wilaya ya Korogwe, kutokana na Bajeti ya
Wizara husika kuwa finyu limeshindwa kufanyiwa marekebisho na kutumiwa vivyo hivyo,
darasa hili halina sakafu wala madawati ya kutosha wanafunzi hukaa chini kwenye
vumbi. Mwalimu aingiapo darasa hutamani wanafunzi wasiinuke kumsalimu maana
vumbi linavyotimka wainukapo ni hatari.
 Mwalimu Mkuu
Shule ya Msingi Msandaka, Manase Kijo akionesha moja ya kitabu cha somo la Tenolojia
ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) anasema somo hili ni changamoto kwa baadhi ya
shule kwani hulazimika kufundishwa na walimu ambao hawana ujuzi wa somo hilo
huku kukiwa hakuna vifaa husika (kompyuta).
 Hapa si
kwamba walimu wameamua kupumzika nje kukimbia joto ofisini ‘No’ Shule hii ya
Msingi Silabu yenye darasa la kwanza hadi la saba haina ofisi ya walimu hivyo
chini ya mti huu wameamua kufanya ofisi ya walimu na pia ofisi ya Mkuu wa
Shule. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Mizeki Charahani akiwa na mwalimu
Julias Mokiwa wa shule hiyo. Hata hivyo kwa sasa kunaujenzi unaendelea ili
kuweka mambo sawa hapo mbeleni.
Mwalimu Mkuu
Shule ya Msingi Msandaka, Manase Kijo akionesha moja ya changamoto ambazo
hukumbana nazo walimu kutokana na mabadiliko ya mara kwa mara ya vitabu vya
masomo bila maandalizi fasaha, shule hiyo ipo katika Manispaa ya Moshi Mkoa wa
Kilimanjaro.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa