Home » » TFDA YASHAURIWA KUFANYA UKAGUZI MIPAKANI

TFDA YASHAURIWA KUFANYA UKAGUZI MIPAKANI

Na Oscar Assenga, Tanga
MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) imeshauriwa kuimarisha mipaka kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa ajili ya kudhibiti uingizwaji wa vipodozi haramu na dawa zilizokwisha muda wake hapa nchini.

Ushauri huo ulitolewa na Kaimu Mfamasia wa Jiji la Tanga, Abdillah Mnenge, wakati wa uteketezaji wa dawa na vipodozi vilivyokwisha muda wake zilizokamatwa kutoka kwa baadhi ya wafanyabishara waliopo mjini hapa.

Dawa, vipodozi na bidhaa za vyakula vilivyotekelezwa vilikuwa na thamani ya Sh 13,908,730 na kati ya hizo, zilizokwisha muda wake zilikuwa na gharama ya Sh 2,356,730, vipodozi vilivyokwisha muda wake vilikuwa na thamani ya Sh 9,263,500 na bidhaa zilizoharibika na kwisha muda wake zilikuwa na thamani ya Sh 2,288,500.

Uteketezaji wa dawa hizo ulifanyika juzi katika dampo lililopo Duga Maforoni, uliosimamiwa na wataalamu kutoka Halmashauri ya Jiji na askari wa Jeshi la Polisi.

Alivitaja bidhaa za vyakula ambavyo vilikamatwa ni vilivyo haribika zikiwamo keki, biskuti, juisi, supu packet, tambi, chumvi na soda za kopo.

Alisema wataendelea kuimarisha zaidi ukaguzi kila baada ya miezi mitatu katika maeneo yote ya Halmashauri ya Tanga kwa ajili ya kudhibiti uingizwaji wa bidhaa zilizokwisha muda.

Chanzo: Mtanzania

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa