na Bertha Mwambela, Pangani
MKUU wa Hifadhi
ya Taifa ya Saadani, Hassan Nguluma, ameiomba serikali kuwasaidia kuwahamisha
wananchi waishio vijiji vilivyopo jirani kutokana na ongezeko la kasi la
uzalianaji wa wanyama hifadhini hapo, hali inayotishia usalama wao.
Akizungumza na
waandishi wa habari waliotembelea hifadhi hiyo mwishoni mwa wiki, Nguluma
alisema kumekuwa na ongezeko kubwa la wanyama kuzaliana, hivyo kufanya eneo la
hifadhi kuwa dogo.
“Tunaomba
serikali itusaidie kuwahamisha wananchi walio jirani na hifadhi, ili tuweze
kupata nafasi ya kutosha kwa ajii ya shughuli za uhifadhi, kwani kwa sasa
kumekua na ongezeko kubwa la wanyama,” alisema Nguluma.
Kwa upande
wake, mkazi wa Kijiji cha Saadani kilichopo jirani na hifadhi hiyo, Rished
Mwinyibabu, alisema anaona kuwa kuna faida kubwa kuwepo kwa hifadhi jirani na
wao kwani hata wale wanyama waliopotea wakati lilipokuwa pori la akiba kwa sasa
wamerudi baada ya kupandishwa hadhi na kuwa hifadhi ya taifa.
Chanzo: Tanania Daima
0 comments:
Post a Comment