Na Oscar Assenga, Tanga
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Luteni mstaafu, Chiku Gallawa, amewataka watendaji katika sekta mbalimbali kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwa ajili kupeleka mbele kasi ya maendeleo.
Akizungumza juzi katika kikao cha viongozi wa mkoa huo juzi, alisema kamwe hatokubali kuwavumilia viongozi wanaoshindwa kuwajibika na kusimamia shughuli zao na kuwa chanzo cha kukwamisha maendeleo ya sehemu husika.
“Utakuta mtu hayupo kazini wiki nzima anafanya shughuli zake na anatumia rasilimali za Serikali, je, watu wa aina hii tutaendelea kuwafumbia macho hadi lini,” alisema Gallawa.
Kuhusu uharibifu unaofanyika katika halmashauri, alisema mtu atakayeonyesha uzembe watachukuliwa hatua za kisheria na hatimaye iwe fundisho kwa watendaji wengine watakaouwa na tabia kama hizo.
Aidha, alisema kutokana na uharibifu wa mazingira unaofanywa na baadhi ya wananchi katika maeneo mbalimbali mkoani hapa, Serikali imeamua kusitisha uvunaji wa misitu pamoja na kugawa mashamba.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, aliwataka watendaji wenzake kuwa makini kwa watu wanaowaongoza kwa ajili ya kufikia malengo waliyojiwekea katika maeneo yao.
Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment