Na Oscar Assenga, Tanga
SERIKALI imeshauriwa kuingiza elimu ya hifadhi ya jamii
katika mitaala ya shule, ili kuwaandaa wanafunzi vyema katika kuchangia mifuko
ya jamii watakapoanza ajira.
Meneja Mfuko wa Hifadhi wa Mashirika ya Umma (PPF) Kanda ya Kinondoni, Pwani na Tanga, Zahara Kayugwa, alitoa wito huo juzi wakati akitoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya Aurora, iliyopo mjini Tanga.
Kayugwa alisema pamoja na kutoa elimu ya hifadhi kupitia vyombo vya habari na vipeperushi, inaonekana bado watu hawajaelewa faida ya kuchangia katika mifuko hiyo.
Meneja huyo alisema mfuko wake tayari umeshaanza kwenda shuleni kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi kabla hawajaingia katika ajira.
Alieleza kuwa mfuko huo sasa hivi umeanza utaratibu wa kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kueleza faida ya wafanyakazi kuchangia katika mifuko hiyo.
Kwa mujibu wa sheria, kila mfanyakazi anatakiwa kujiandikisha katika mifuko ya jamii bila kujali yuko katika ajira ya aina gani.
Wakati huo huo, Kayugwa aliwataka wanachama wa mifuko ya jamii kuwa na subira kwa kiasi cha miezi sita, wakati ambapo kamati maalumu ya wataalamu kutoka katika mifuko ya jamii inakusanya maoni na kuandaa utaratibu unaofaa kwa ajili ya sheria mpya ya mafao.
Kwa mujibu wa sheria ya sasa ya mafao ya mifuko hiyo, mwanachama haruhusiwi kuchukua mafao yake kama hajafika umri wa miaka 55.
Alisema ni kweli kuna aina ya ajira ambapo kumtaka mtu asilipwe mafao hadi umri huo wa miaka 55 ni kumsababishia mateso.
Aliwaambia wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwa kamati itaangalia ni ajira za aina gani ambazo zinastahili kusubiri na zile ambazo hazistahili kusubiri.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment