Na Bakari Kimwanga, Pangani
MBUNGE wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), amekabidhi mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Kijiji cha Kipumbwi kujenga shule ya msingi.
Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo jana, alisema kuweza kujenga jamii imara ni lazima kuhakikisha elimu inapewa kipaumbele cha pekee.
“Sina budi kuunga mkono juhudi zenu za ujenzi wa Shule ya Kipumbwi Mtoni, ambayo imejengwa kwa nguvu za wananchi, nami kama mwakilishi wetu ninaungana nanyi kwa dhati na katika hili napenda kukabidhi mifuko ya saruji.
“Kwa kipindi cha siku kadhaa nimekuwa na ziara katika Mkoa wa Tanga, lakini nilipofika katika Kijiji cha Mkwaja hali ni mbaya, shule yenye wanafunzi zaidi ya 300 lakini ina walimu wanne tu.
“Mbali na hali hiyo, kati ya watoto hao, watoto 283 wa darasa la kwanza hadi la saba hawajui kusoma wala kuandika, je, hapa wa kulaumiwa ni nani. CCM imeshindwa kusimamia sera ya elimu kwa vitendo na sasa hawana budi kuadhibiwa nanyi wananchi kutokana na hali hii.
“Serikali imekuwa haina mpango katika kuinua elimu kwa kuwa imekurupuka katika ujenzi wa shule za sekondari za kata, hali ya kuwa haina mpango wa kuajiri walimu wengi zaidi.
“Hata walimu waliopo kila kukicha ni matatizo na Serikali ambayo kwa muda mrefu iliahidi kulipa madai yao, lakini hadi leo wameshindwa, hali inayosababisha walimu kuadhibu watoto kwa kutowapa elimu bora darasani,” alisema Mwidau.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kipumbwi, Jamali Nassoro, alimshukuru mbunge huyo kwa kuunga mkono juhudi za wananchi za kuinua sekta ya elimu wilayani Pangani.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment