Na Bakari Kimwanga, Tanga
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CUF), Amina Mwidau, amekabidhi mabati kwa kikundi cha Gongagonga cha Mwanzange pamoja na vifaa vya michezo kama njia ya kuwawezesha wajasiriamali.
Akizungumza mjini hapa juzi baada ya kukabidhi mabati hayo kwa Diwani wa Kata ya Mwanzange, Rashid Jumbe (CUF), alisema Taifa haliwezi kuendelea bila kuandaa utaratibu mzuri wa kuwathamini wajasiriamali wadogo wadogo.
Alisema mabati hayo kwa kikundi hicho ni sehemu ya ahadi yake kwa wajasiriamali hao ambao walitaka wapatiwe waweze kujenga banda, litakalowasaidia kuwakinga na jua pamoja na mvua.
“Ninajisikia furaha kutoka ndani ya nafsi nyangu kuweza kuwakabidhi mabati haya yenye thamani ya shilingi 170,000, nanajua huu ni mwanzo najua tutakutana tena kuweza kutekeleza na mengine zaidi.
“Kama mnavyofahamu kuwa Taifa lolote liweze kuendelea ni lazima liandae mazingira mazuri kwa wajasiriamali wake hasa vijana na wanawake ambao ndiyo nguvu kazi ya Taifa na kama nilivyokuja na kuniambia niwaletee nini sasa nimeanza na utekelezaji wa ahadi yangu hii kwenu.
“Mbali na hatua hii, sasa ninachowaomba anzeni harakati za kusajili Saccos na hatimaye muweze kukopesheka na taasisi za fedha nami nitawasaidia kwa kulisimamia hili kwa nguvu zangu zote,” alisema Mwidau.
Kwa upande wake, Jumbe, alimshuruku mbunge huyo kutekeleza ahadi yake kwa wakati huku akiamuahidi atahakikisha anasimamia utekelezaji wa uanzishwaji wa Saccos kwa wajasiriamali wa Gongagonga.
“Ninajua wapo wengi lakini mbunge wetu Mwidau, umeonyesha mfano wa kuigwa, kwa kuwa umeweza kutekeleza hili katika kipindi kifupi tangu ulipokuja hapa na kuzungumza na wajasiriamali,” alisema Jumbe.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment