Home » » HALMASHAURI TANGA YAINGIA UBIA KUFUFUA VIWANDA

HALMASHAURI TANGA YAINGIA UBIA KUFUFUA VIWANDA

Mwandishi wetu, Tanga Yetu

KAMPUNI ya  Tanga ECONOMIC Corridor LTD ni kampuni iliyoingia ubia na Halmashauri ya jiji la Tanga kwa lengo la kufufua viwanda na uchumi wa mkoa wa Tanga ili kuongeza kasi ya maendeleo na biashara mbalimbali zitakazo ambatana na uwanzishwaji wa mradi huo.
Akikabidhi  hati ya mradi huo kwa mkurugenzi wa kampuni hiyo Tanga ECONOMIC Corridor  Mstahiki  Mea  wa jiji la Tanga Bwana Omari Guledi amesema kukamilika kwa mradi huo kutasidia kuwezesha upatikanaji wa ajira mpya kwa wakazi wa jiji la Tanga pamoja na kuongeza huduma mbalimbali za kijamii na makusanyo ya kodi katika mkoa wa Tanga.
Aidha mstahiki mea wa jiji la Tanga Bwana Guled ameeleza kwamba mpaka sasa kampuni ya Tanga Economic Corridor inasubiri kibali cha kuanzishwa mpango maalumu wa eneo la kiuchumi kutoka Mamlaka ya EPZA iliyoko chini ya wizara ya viwanda na biashara.
Hata hivyo Mh Mstahiki mea wa jiji la Tanga ameongeza kwamba Mpango huo maeneo maalumu  ya kiuchumi utawezesha bidhaa zitakazozalishwa na viwanda mbalimbali chini ya mradi huu,kuweza kuuzwa hapa nchini nan je ya nchi,hususa ni nchi za barani afrika.
Kwa upande wake mkurungenzi wa kampuni hiyo Bwana Chris Chae ambaye ni muwekezaji kutoka nchini Korea ameshukuru kukabidhiwa hati hiyo nakwamba wao wanania na dhamira ya kuendeleza viwanda pamoja na kufufua ili kuisapoti serikali katika mkoa wa Tanga.
JUMLA ya viwanja 68 vimetengwa katika eneo la Pongwe nje kidogo ya jiji la Tanga kwa wawekezaji na makazi.
Blogzamikoa

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa