Home » » WANAOSAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU WAKAMATWA TANGA

WANAOSAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU WAKAMATWA TANGA




Na Oscar Assenga, Tanga

WAFANYABIASHARA 11 wanaojishughulisha na biashara ya kuwasafirisha wahamiaji haramu mkoani Tanga wamekamatwa na Idara ya Uhamiaji katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Julai, 2012.

Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, Sixtus Nyaki, alisema wafanyabiashara hao wamekuwa wakijihusisha kwa kuwaingiza wahamiaji hao na kuwahifadhi katika maeneo mbalimbali pindi waingiapo.

Aliwataja waliokamatwa na maeneo wanayotokea kuwa ni Abdallah Yasin (Dar es Salaam), Amiri Saidi (Dar es Salaam), Jambia Omari (Dar es Salaam), Charles Munuo (Dar es Salaam), John Mfinanga (Dar es Salaam), Hussein Bonguemura (Dar es Salaam), Shabani Maingu (Dar es Salaam), Philio Langeni (Dar es Salaam), Hassani Shehe (Kenya), Iddy Hingu (Dar es Salaam) na Nile Tashoma (Ethiopia).

Alisema baada ya kuwakamata waliwapeleka mahakamani na kupigwa faini na kuachiliwa na baadhi yao wakiendelea kushikiliwa ambao ni Hassani Issack, Iddy Hingu na Nile Tashoma ambapo wapo rumande na kesi zao zipo mahakamani na uchunguzi unaendelea. 

Alisema changamoto kubwa inayowakabili ni mipaka mingi kuwa wazi na wananchi kushirikiana na wasafirishaji hao na kusababisha operesheni zao kuwa ngumu.


Chanzo: Mtanzania


0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa