WAKAZI wa Jiji la Tanga wametakiwa kukitumia kituo kipya cha mabasi yaendayo mikoani na wilayani kilichopo Kange ingawa
bado kuna baadhi ya changamoto za kukamika kwake.
Rai hiyo ilitolewa na Mstahiki Meya wa Jiji hilo, Omary Gulledy
alipozungumza na madiwani katika kikao cha baraza kilichofanyika jijini
hapa.
Alisema wakazi wa Tanga wasione kimya katika umaliziwaji wa kituo
hicho bali ni serikali inaendelea na mchakato wa kufikisha huduma zote
muhimu kwenye stendi hiyo mpya.
Sambamba na hayo Gulledy alisema lengo hasa la kuhamishia stendi hiyo
Kange ni kulikuza jiji baada ya kituo cha mabasi kilichokuwepo kuwa
kidogo.
Kwa upande wake Naibu Meya wa jiji hilo Mzamini Shemdoe alisema kuna
mipango ya muda mfupi na mrefu kwa ajili ya kujenga vibanda vya biashara
vya muda ili kukidhi mahitaji ya wasafiri na wakazi kwa ujumla.
Chanzo;Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment