Home » » Maofisa Habari na Mawasiliano wa Serikali Watembelea Kituo cha Wazee Tanga

Maofisa Habari na Mawasiliano wa Serikali Watembelea Kituo cha Wazee Tanga

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy (mwenyeshati la mistari) na Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni toka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko (katikati) wakimkabidhi  kiroba cha mchele moja ya Wazee wa Kituo cha Mwanzange Mkoani Tanga, ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali katika kikao kazi kinachoendelea Mkoani humo.

Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni toka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko akimkabidhi Afisa Ustawi wa Jamii anayesimamia kituo hicho cha wazee Bi Otilia Daniel fedha za kununulia mahitaji mengine wakati wa ziara ya kutoa msaada katika kituo hicho leo Mkoani Tanga.
Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni toka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko akimkabidhi Afisa Ustawi wa Jamii anayesimamia kituo hicho cha wazee Bi Otilia Daniel fedha za kununulia mahitaji mengine wakati wa ziara ya kutoa msaada katika kituo hicho  Mkoani Tanga.
Maofisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wazee wa kito cha Mwanzange ambapo walitoa Unga sembe Kilo 200,mchele kilo 300,mafuta ya kupikia dumu 2,mafuta ya kupaka, dawa za meno, chumvi, sukari, maharage, nyama, majani ya chai, kanzu, misuli pamoja na nguo za kinamama. (Picha Na Hassan Silayo)

The habari .com

1 comments:

Unknown said...

Ni busara kuwatembea wazee, kwani wanapata matumani ya kuwa tunawajali pamoja na kupata upendo kutoka kwa vijana wao. hata na hivyo hatuna budi kuangalia namna bora ya kuwasaidia wazee wasiojiweza, ni lazima tukumbuke hata na sisi tutakuwa wazee kwa atajayejaaliwa umri mrefu. Mr. Shariff

Post a Comment

Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa