Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem (kushoto) akimkabidhi mabeseni 50 yenye vifaa tiba kwa ajili ya akina mama wajawazito na watoto wachanga, Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhina Mustapha Selebosi ,kulia
Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem atia saini katika kitabu cha wageni mara alipowasili katika uzinduzi wa Kisima
Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem amezindua visima sita vya maji safi na salama katika Mkoa wa Tanga mwisho wa wiki,ikiwemo shule ya Old Tanga Secondary School vilivyochimbwa na Jumuiya ya Direct Aid ya Kuwait ikiwa ni mwendelezo wa mradi ulioanzishwa na Ubalozi huo.
Balozi
wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem amezindua visima sita vya maji
safi na salama mwisho wa wiki katika Mkoa wa tanga ikiwemo shule ya Old
Tanga Secondary School ,vilivyochimbwa na Jumuiya ya Direct Aid ya
Kuwait ikiwa ni mwendelezo wa mradi ulioanzishwa na Ubalozi wa Kuwait
nchini unaofahamika kwa jina la “KISIMA CHA MAJI KATIKA KILA SHULE”,
uzinduzi ambao ulihudhuriwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhina
Mustapha Selebosi, walimu, wanafunzi na wadau mbalimbali.
Aidha
Balozi wa Kuwait alitembelea kituo cha afya cha Ngamiani ambapo
alimkabidhi Mstahiki Meya wa Tanga mabeseni 50 yenye vifaa tiba kwa
ajili ya akina mama wajawazito na watoto wachanga, mabeseni ambayo ni
msaada kutoka taasisi ya Red Crescent ya Kuwait. Akiwa mjini Tanga
Balozi Al-Najem alihudhuria mahafali ya kuhitimu wanafunzi wa Shule ya
sekondari ya Kheri ya wanawake.
Kwa
upande wake Meya wa Tanga aliushukuru Ubalozi wa Kuwait nchini kwa
msaada huo na akamuomba Balozi wa Kuwait pia aweze kusaidia katika shule
za jiji hilo 98 za msingi na 32 za sekondari Rkupata huduma ya visima
vya maji.
0 comments:
Post a Comment