Home » » UNCDF YAISAIDIA ENSOL KUPELEKA UMEME VIJIJINI

UNCDF YAISAIDIA ENSOL KUPELEKA UMEME VIJIJINI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  

 Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mhandishi Robert Gabriel (kushoto) akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt Juliana Pallangyo kuzindua rasmi mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme wa 48KW kwa teknolojia ya nishati ya jua katika kijiji cha Mpale wilayani Korogwe, mkoa wa Tanga.
 Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji na Maendeleo (UNCDF) nchini, Peter Malika akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa rasmi wa mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme wa 48KW kwa teknolojia ya nishati ya jua katika kijiji cha Mpale, wilayani Korogwe mkoa wa Tanga.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Juliana Pallangyo akitoa nasaha wakati wa uzinduzi rasmi wa mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme wa 48KW kwa teknolojia ya nishati ya jua katika kijiji cha Mpale wilayani Korogwe, mkoa wa Tanga. Kulshoto ni Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji na Maendeleo (UNCDF), Peter Malika. 

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji na Maendeleo (The United Nations Capital Development Fund-UNCDF), ikishirikiana na kampuni ya Ensol Tanzania Ltd. (Ensol) wamezindua mfumo wa umeme wa nishati ya jua katika kijiji cha Mpale kilichopo wilaya ya Korogwe, na hivyo kuwezesha umeme katika eneo hilo kwa mara ya kwanza. 

Mradi huo ulizinduliwa rasmi na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dk. Juliana Pallangyo ambaye aliipongeza kampuni ya Ensol na washirika wake ikiwemo UNCDF kwa juhudi zake kubwa za ushawishi wa umeme hasa umeme mbadala wa jua ili kuboresha ustawi wa jamii na kukuza uchumi wa mtu binafsi na taifa. 

Dk. Pallangyo alisema kwamba serikali ya Tanzania inawashukuru watu wa Ensol kwa juhudi zao kubwa za kupeleka umeme vijijini. Alisema kwa Ensol kuweza kufikisha umeme katika maeneo ya ndani kabisa ya kijiji cha Mpale, kuwaunganisha wananchi na umeme wa saa 24 na wamefanikiwa kubadili maisha ya wananchi hao. 

 Alitoa wito kwa jumuiya hiyo kutumia umeme sio kwa kuwasha taa pekee bali pia katika kusukuma mbele kazi za uzalishaji. Dk. Pallangyo alifurahishwa na kituo cha afya Mpale kuunganishwa na mfumo wa nishati ya jua na kuwataka maofisa wa wilaya kulipa Ankara zao kwa wakati ili kuhakikisha kwamba huduma zinapatikana bila kukoma kwa wananchi. 

Kijiji cha Mpale kipo katika maeneo ya milimani katika kata ya Mpale wilaya ya Korogwe mkoani Tanga. Kijiji chenye wakazi 9000 na nyumba 730, tangu kuanzishwa kwake mwaka 1972 hakijawahi kuwa na umeme. Wengi wa wanavijiji walikuwa wakitegemea mno mafuta ya taa ambayo kwa kiasi kikubwa yalikuwa si masafi kwa ajili ya kuwashia taa zao.

Mpaka sasa Ensol imeshaunganisha umeme kwa kaya 50. Aidha mpango unafanyika wa kutanua mradi ili ifikapo Juni 2018 nyumbna 250 ziwe zimeunganishwa. Mreadi huo wa kuunganisha wanakijiji na nishati inayozalishwa kwa nguvu za jua ulianza mwaka 2014 wakati Ensol walipozuru vijiji kadhaa vya mkoa wa Tanga kuangalia uwezekano wa kupata kijiji cha mfano na kubaini kuwapo kwa kijiji cha Mpale. 

“Ushirikiano wa UNCDF ulikuwa muhimu katika mradi huu gridi ndogo ya nishati ya jua. Pamoja na kwamba tulipokea fedha kutoka UNCDF na wadau wengine, UNCDF imekuwa ndio chombo cha kuingiza masuala ya kitaalamu na ushauri mwingine. Kushirikiana na UNCDF kumeongeza kuaminika miongoni mwa wadau na taasisi za kifedha,” anasema Prosper Magali, Meneja wa mradi wa Mpale.

Bw. Magali aliongeza, "Ninaamini kama si msaada wa UNCDF huu mradi usingekuwepo hapa ulipo. Tumepokea fedha kutoka EEP na wafadhili wengine. Lakini ni kwa sababu ya UNCDF tumeweza kupata fedha kutoka katika taasisi nyingine za ufadhili". Mkuu wa UNCDF Tanzania, Peter Malika alisema kwamba umeme ni chanzo cha maendeleo na kwamba sekta binafsi ina nafasi ya kusaidia serikali katika juhudi zake za kuangaza maeneo ya vijijini. 

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa