Home » » HOSPITALI YA TEULE MUHEZA YAPATIWA MSAADA WA MASHUKA

HOSPITALI YA TEULE MUHEZA YAPATIWA MSAADA WA MASHUKA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Boniface Mhabe kushoto akipokea msaada wa mashuka 50 kutoka kwa Afisa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Sub Agro Trading anda Engineering,Neema Ng'unda kwa ajili ya wodi ya wakina mama wajawazito kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza jana ilkiwa ni kutambua mchango mkubwa wa wanawake katika kilimo wa pili kutoka kushoto ni   Afisa  Mauzo wa Suba Agro Trading yenye makao makuu yake mjini Arusha,Shillaga Samweli 

HOSPITALI ya Teule wilayani Muheza Mkoani Tanga imepata msaada wa mashuka 50 kwa ajili ya kukabiliana na uhaba uliopo kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wagonjwa wanao kwenda kupata matibabu kutoka maeneo mbalimbali hasa vijijini.

Hatua ya uhaba huo unatokana na uchakavu wa wa mashuka unaotokana na
  kufubaa unaosababishwa na maji wanayotumia kufulia kutokana na uhaba wa maji hali iliyopelekea kuwepo uhitaji kila wakati ili kuweza kukithi mahitaji ya wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu.

Hayo yalibainishwa jana na Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,
  Boniphace Mhabe wakati akipokea msaada wa mashuka 50 kutoka kampuni ya Suba Agro Trading na Engineering ambao ni mzalishaji wa mbegu bora zamahindi kwa kushirikiana na Cimmity taasisi ya kimataifa ya utafiti wa mahindi na Ngano.

Shuka hilo zilitolewa kwa ajili ya wodi ya wakina mama wajawazito
  kwenye hosptali ya Teule Muheza,Hospitali ya wilaya ya korogwe na ile ya wilaya ya Handeni lengo kubwa likiwa kuwaondolea changamoto zinazowakabili.

"Vitanda vipo vingi lakini tatizo kubwa ni mashuka na hili linatokana
  na asilimia kub wa kuchakaa kutokana na maji lakini pia wakati mwengine yanabadilika rangi jambo ambalo limekuwa changamoto kwao.

Aidha alisema wanaishukuru kampuni hiyo kwa kuona umuhimu wa kusaidia
  msaada huo ambao umefika wakati muafaka kwa kusadia baadhi ya vikwazo wanazokutana navyo wakati wa utoaji wa huduma  za afya.

Awali akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo,Afisa Masoko na
  Mauzo wa Kampuni hiyo,Neema Ng'unda alisema alisema wamekuwawakishiriki katika kuhamasisha kilimo Tanzania hususani kwa wakina mama ambao ndio nguzo kubwa hapa nchini kufikia mafanikio.

Alisema wamelenga wanawake kwa sababu ndio muhimili muhimu kwenye
  jamii wa kuwawezesha wakina baba kwenye kulima kilimo bora ambapo kinaweza kuwainua kiuchumi.

"Lakini pia tunawashukuru wakulima wote Tanzania kwa kutumia mbegu zao
  kwa kulima kilimo cha kisasa ambacho kinaweza kuwa mkombozi kijiinuakimaendeleo na kukuza mitaji yao "Alisema.

Naye kwa upande wake,Afisa Mauzo wa Suba Agro Trading yenye makao
 makuu yake mjini Arusha,Shillaga Samweli alisema zoezi hili limelenga kurudisha fadhila kwa wakina mama wa Tanzania maana ndio wamekuwa wakishiriki kikamilifu katika kilimo.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa