Tanga,
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Deudence Kakoko,
amewataka wafanyakazi wa mamlaka hiyo kufanya kazi kwa bidii ili kwenda
kasi ya Serikali ya awamu ya Tano.
Akifungua
michezo ya Tano ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (INTERPORTS
GAMES) viwanja vya shule ya Sekondari ya Popatlal Tanga jana, Kakoko,
alisema kila mfanyakazi wa Mamlaka hiyo anapaswa kujua wajibu wake.
Alisema
kasi hiyo iende sambamba na uboreshaji wa utoaji huduma bandarini na
kuwa kivutio kwa wageni ili kuweza kuitumia kwa kushusha shehena zao
bandari za Tanzania.
Michezo hiyo inashirikisha wafanyakazi wachezaji kutoka Tanga ambao ni wenyeji, Dar es Salaam,, Mtwara na Bandari za Ziwa.
0 comments:
Post a Comment