Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Tanga,
KIWANDA Cha Saruji Cha Simba Cement kimeijengea shule ya Msingi ya
Kange vyumba viwili vya madara na madawati 50 pamoja na matundu mawili
vya vyoo vyote vikiwa na thamani zaidi ya shilingi milioni 76.
Msaada
huo umekuja kupunguza kero ya wanafunzi kurundikana darasa moja na
wengine kukaa chini jambo ambalo hupunguza ufahamu wa wanafunzi
darasani.
Akizungumza
katika hafla fupi ya makabidhiano, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias
Mwailapwa, alisema msaada huo uwe mfano kwa makampuni mengine na wadau
wa elimu lengo likiwa ni kuondokana na changamoto ya baadhi ya shule inazokabiliana nazo.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Rasilimali watu kiwanda cha Saruji cha Simba
Cment, Anna Malambugi, alisema kiwanda hicho moja ya sera zake ni
kusaidia jamii ikiwemo, Elimu, Afya na Mazingira.
Nae
Mwalimu mkuu wa Shule hiyo, Debora Danniel, alisema awali walikuwa
wakiwaweka wanafunzi 120 darasa moja kufuatia uhaba wa madarasa.
Alisema
kwa msaada huo utaondosha kero ya wanafunzi kurundikana darasa moja na
kuwaomba wadau wa elimu kuisaidia shule hiyo katika Nyanja mbalimbali
ikiwemo miundombinu yamaji na uchakavu wa majengo.
Mwisho
Mkuu
wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwailapwa akifungua moja milango ya vyumba
viwili ya madarasa shule ya msingi Kange Tanga, anaemtazama ni Afisa
Fedha Pitter De Jagger na kulia ni Mkurugenzi wa jiji la Tanga, Daudi
Mayeji.
Afisa Uhusiano kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga, Noor Mtanga, akiwakabidhi madawati 50 wanafunzi wa shule ya msingi ya Kange pamoja na majengo mawili na vyoo vyenye matundu mawili vyote vikiwa na thamani zaidi ya shilingi milioni 76, nyuma kulia ni Mwenyekiti wa mtaa wa Kasera, Aidan Munis na kulia ni mwalimu mkuu wa shule hiyo, Debora Mzava.
Mkuu Rasiliwamali watu kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga, Anna Mwalambuji akiwakabidhi madawati 50 wanafunzi wa shule ya msingi ya Kange kufuatia uhaba wa madawati shule hiyo pompja na kuwakabidhi jengo la vyumba viwili na vyoo vyenye matundu mawili vyote vikiwa na thamani zaidi ya shilingi milioni 76.
0 comments:
Post a Comment